Albert Mangwea. |
Taarifa zilizopatikana mapema leo kutoka Afrika Kusini ambapo inasemekana msanii huyo alikuwa akiishi, zinasema Ngwair alifikwa na umauti mapema leo.
Akizungumza na mwandishi, mmoja wa watanzania anayeishi Johannesburg, Afrika Kusini, Ramadhan Mnyanga alisema Ngwair alikutwa na umauti kwenye hospitali ya St Hellen mjini hapo.
“Mwenzake anayekaa naye anaitwa Kem anasema leo (jana) alirudi geto kwao (nyumbani) usiku akiwa mzima tu wakapata chakula wakalala alipoamka asubuhi Ngwea alikuwa bado kalala akaamua kuondoka zake asimsumbue, lakini akiwa kwenye pilika zake akapigiwa simu na wenzake kwamba mshikaji ana hali mbaya, akarudi na kumpeleka hospitali na hivi ninavyozungumza na wewe tumetoka hospitali wamethibitisha kwamba amefariki," alisema Mnyanga.
Hata hivyo, haijajulikana mara moja sababu ya kifo cha Mangwea ambaye alikuwa mmoja wa wasanii kutoka 'East Zoo'.
Mangwea alianza kujulikana kwenye ulimwengu wa muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 na nyimbo zake zilizomtambulisha vilivyo na kujizolea mashabiki wa muziki ni Mikasi na Gheto Langu.
No comments:
Post a Comment