HUYU NDIYE KIKONGWE KABISA ANAYEISHI DUNIANI ALIYEZALIWA KARNE YA 19...

Jiroemon Kimura alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni.
Japo bado kuna wanawake 21, lakini katika umri wa miaka 116 ni mtu wa mwisho aliye hai.

Baada ya kifo cha James Emmanuel 'Doc' Sisnett huko Barbados, akiwa na umri wa miaka 113 na siku 90, mtu mzee zaidi anayeishi duniani Jiroemon Kimura ni mtu wa mwisho aliye hai ambaye alizaliwa katika karne ya 19.
Mjapani mfanyakazi wa zamani wa post Kimura, ambaye alizaliwa Aprili 19, 1897, alitajwa na Rekodi za Dunia za Guinness kuwa mtu mzee kabisa duniani baada ya kifo cha mwanamke wa Kimarekani, Dina Manfredini mnamo Desemba 17, 2012.
Sasa, kwa mujibu wa Kundi la Utafiti la Gerontolgy la UCLA, ni yeye pekee na wanawake 21 waliozaliwa kabla ya Siku ya Mwaka Mpya, 1901, ambao bado wanaishi katika sayari hii, imeripotiwa.
Wengi wao wanaishi nchini Marekani au Japani, huku wengine wakiwa barani Ulaya na Canada. Supercentenarian alizaliwa Aprili 19, 1897.
Supercentenarian ni watu ambao wameishi zaidi ya miaka 110, na wakati imekadiriwa kwamba kuna pengine 200 au 300 wanaoishi hadi leo, huku wasiozidi 60 wakiwa wamehakikiwa kwa kutumia kumbukumbu zinazoaminika.
Kati yao wawili tu, Kimura na mwanamke wa Kijapani Misao Okawa, ndio wanaofahamika kuwa bado wako hai wakiwa na umri wa miaka 115 au zaidi.
Akiwa amezaliwa katika miaka 30 ya kipindi cha Meiji, Kimura ameishi katika utawala wa wafalme wanne, na chini ya uongozi wa mawaziri wakuu 61 wa Japani, kuanzia Matsukata Masayoshi hadi Shinzo Abe.
Kimura alistaafu mwaka 1962 akiwa na umri wa miaka 65, baada ya kufanya kazi kwa miaka 45 kwenye ofisi ya posta nchini Japani.
Kwa sasa anaishi huko Kyotango, Kyoto Prefecture, mjane wa mtoto wake mkubwa wa kiume, mwenye miaka 83, na mjane wa mjukuu wake wa kiume, mwenye miaka 59, na akiendesha maisha yake marefu kwa kula sehemu ndogo ya chakula, na kutumia muda wake mwingi 'kitandani'.
Kaulimbiu ya Kimura katika maisha na siri ya kuishi muda mrefu ni 'kula kidogo na kuishi muda mrefu', alisema ofisa mmoja.
Kamura havuti sigara, hunywa kiasi 'kiduchu' cha pombe, na amejizoesha kula hadi kufikia asilimia 80 kabla ya kushiba kabisa.
Kizee hicho kina wajukuu 14, vitukuu 25 na watoto wa vitukuu 13, na alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa pamoja na ndugu zake.
Taji lake kama mtu mzee zaidi kuishi duniani kwa sasa linapiganiwa na mwanamke wa China, Luo Meizhen, mwanamke ambaye anadai kuwa anatimiza miaka 127 ifikapo Septemba.
Lakini Luo hana cheti cha kuzaliwa kuthibitisha umri wake, huku akiwa tu na kitambulisho kinachoeleza kwamba alizaliwa mwaka 1885.

1 comment:

Anonymous said...

Good blog you have here.. It's difficult to find excellent writing like yours nowadays.

I honestly appreciate people like you! Take care!!