JUU: Postamasta Richard Gates akiwa mbele ya duka hilo. KUSHOTO: Duka hilo baada ya kufanyiwa ukarabati miaka takribani 50 iliyopita. KULIA: Duka hilo enzi hizo. |
Limekuwa hapo kwa miaka 600, lakini hatima ya duka kongwe kabisa nchini Uingereza imeingia mashakani jana baada ya kutangazwa kuuzwa.
Wanahistoria wamegundua ofisi hiyo ya posta na duka kwenye jamii ndogo ya Boxford, Suffolk, ambalo hapo awali lilitumika kama ghala la kuuza na kununua sufu na vitambaa miaka mingi iliyopita ya hadi 1420.
Kwa zaidi ya karne zilizofuatia jengo hilo limekuwa mahali pa wauza nyama, vyakula, wahunzi na wauza nguo na tangu kuanza kwa karne iliyopita imekuwa maarufu kama duka la vitu mbalimbali na ofisi ya posta.
Kwa mlingano, kijiji hicho pia ni mahali ilipo gereji kongwe zaidi nchini Uingereza ya Riddelsdells, lakini hatima ya moja ya biashara zinazoheshimika sasa iko mashakani baada ya mmiliki wa kijiji hicho mwenye umri wa miaka 94 kufariki na wasimamizi wake wa mirathi wameliingiza sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Postamasta mdogo Richard Gates alisema: "Wote tunatumaini mmiliki huyo mpya ataliendeleza duka hili, kumekuwa na vivutio vingi mno katika maduka haya - itakuwa muafaka kwa yeyote kama mtu wa benki iliyoteketea ambaye anataka kufanya kitu kingine.
Imekuwa sehemu ya alama za kijiji na tunapata wateja ambao wamekuwa wakija hapa katika maisha yao yote.
"Walianza kama watoto kununua pipi wakiwa njiani kwenda shule na sasa wanakuja kuchukua pensheni zao za uzeeni mahali hapa."
Gates, mwenye miaka 68, ambaye amekuwa meneja wa ofisi hiyo ndogo ya posta kwa miaka 15, aliongeza: "Vitu vingi unavyohitaji katika maisha vinaweza kununuliwa katika kijiji hiki - tuna duka la karatasi, bishaa mchanganyiko na nyama.
"Ofisi za posta za jirani ziko umbali wa takribani maili 6 kutoka hapa kuelekea pande zote hivyo utapenda kuona likiendelea kuwapo - na ningependa kuendelea kusimamia ofisi hii ya posta."
Lakini jengo hilo lenye vyumba vitano linahitaji ukarabati mkubwa - hakuna kilichofanyika hapo tangu lililonunuliwa na Meja mstaafu wa jeshi, John Gaussen na mkewe, Christina miaka 50 iliyopita.
Kama ilivyowekwa kwenye orodha ya Daraja la Pili kwa majengo ya biashara, mabadiliko yoyote ya matumizi yanatakiwa kuthibitishwa na halmashauri ya wilaya hiyo - ambayo ina mamlaka ya usimamizi wa utunzaji wa muonekano wa majengo ya kale.
Meja Gaussen alifariki mwaka 1997 na mkewe alifariki miaka minane iliyopita akiwa na umri wa miaka 89 ndipo duka hilo likaachwa mikononi mwa dada mkubwa wa Christina, Catherine Lee, mseja anayeishi mjini Lavenham, maili nane kutoka hapo.
Alimruhusu kuendesha sehemu hiyo lakini sasa baada ya kifo chake miezi 15 iliyopita akiwa na umri wa miaka 94, wasimamizi hao wa mirathi wanakusudia kupauza na kufidia shamba lake.
Jengo hilo lililojengwa kwa mbao sehemu kubwa - ambalo limebadilika kiasi kwa muonekano kwa karne kadhaa, pia lina ghala maarufu la nafaka lenye ghorofa mbili.
Mapema kwenye karne ya 20 Buck Riddleston - ambaye familia yake pia ilimiliki gereji kijijini hapo - aliongeza uwigo wa bidhaa zinazouzwa hapo ikiwamo nguo, mavazi, mashati na soksi ndefu.
Hatahivyo Boxford Stores sasa iko sokoni na idadi ya wakazi wa kijiji hicho ya watu 1,200 ina wasiwasi na kutumaini kwamba litaendelea kuwa katika hali yake ya sasa kama duka la deli, matunda na mboga za majani na ofisi ndogo ya posta.
Boxford, mahali ambapo mapadri mahujaji waliondoka na kwenda Marekani mwaka 1620, pia inajivunia gereji kongwe zaidi nchini Uingereza - wakati fulani ikiwahi kusimamiwa na familia hiyo ambayo ilimiliki maduka kwenye ofisi hiyo ya posta.
Riddelsdells ilianzishwa mwaka 1960 huku ikishughulikia magari yaliyokuwa yakiendeshwa kwa mvuke na mikokoteni ya mashambani.
No comments:
Post a Comment