SHUSHUSHU WA KIKE ASIMULIA ALIVYOTEGA BOMU NA KUUA WATU 115 KWENYE NDEGE...

Kim Hyun-hee
Shushushu wa zamani wa kike Korea Kaskazini amebainisha jinsi alivyonyakuliwa kutoka katika familia yake ili kutumikia taifa hilo lenye usiri mkubwa - kisha kutakiwa kulipua ndege ya abiria ambayo iliuawa watu 115.

Kim Hyun-hee, ambaye alijaribu kujiua kwa sumu baada ya kuwa amekamatwa na Wakorea Kusini na baadaye kukwepa adhabu ya kifo, amezungumza hadharani kujaribu kuwashambulia mabosi zake wa serikali ya zamani ya Kikomunisti kama wachochezi wa vita.
Akizungumza kutokea mafichoni nchini Korea Kusini, gaidi huyo wa zamani mwenye miaka 51 alisema anaamini vitisho vyote vya hivi karibuni kutoka Pyongyang si chochote zaidi ya jaribio la kutafuta kuungwa mkono kwa kiongozi mpya kijana, Kim Jong-un.
"Kim Jong-un ni kijana mno na mwenye uzoefu mdogo mno," alisema. "Anahangaika kupata mamlaka kamili dhidi ya jeshi hilo na kushinda utiifu wao.
"Ndio maana anafanya ziara nyingi kwenye makao makuu ya jeshi - kuweza kupata kuungwa mkono." Alisema kulikuwa na sababu nzuri kwa Kaskazini kutishia kuanzisha vita vya makombora ya nyuklia.
"Korea Kaskazini imetoa mpango wake wa nyuklia kuwaweka watu wake katika mstari na kuisukuma Korea Kusini na Marekani kukubali."
Anaishi katika hofu kwamba wauaji wa Korea Kaskazini watajaribu kumfikia aliko na kumdhibiti asisambaze taarifa za ndani kuhusu taifa hilo la Kistalini ambalo aliwahi kulitumikia kwa uaminifu mkubwa.
Mnamo mwaka 1987 alipewa amri kutoka kwa kiongozi wa wakati huo Kim Jong-il kulipua ndege namba KAL 858.
Yeye na wakala mwingine, Kim Seung-il, ambaye alikuwa kama baba yake, walisafiri kwa kutumia ndege ya Korea Kusini kupitia Ulaya na kuelekea Bahrain, kuteremka baada ya kutega bomu la plastiki, waliloficha kwenye mtambo wa redio, katika sehemu ya mizigo.
Mlipuko huo baadaye ukaipeleka ndege hiyo ikiporomoka kwenye msitu mnene karibu na mpaka wa Thai-Burma, na kuua kila mtu aliyekuwa ndani.
Shambulio hilo la mwaka 1987 liliua watu 115 waliokuwamo kwenye ndege hiyo na kuipelekea Marekani kuiorodhesha Korea Kaskazini kama taifa linalofadhili ugaidi.
Baada ya kukamatwa huko Bahrain kwa kumiliki pasipoti zilizoghushiwa, 'baba' huyo akajiua mwenyewe kwa vidonge lakini Kim, ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 wakati huo, hakufanikiwa katika jaribio lake la kutaka kujiua.
Akiwa amehukumiwa hukumu ya kifo na mahakama ya Korea ya Kusini, baadaye alisamehewa na kwenda kuishi sehemu hiyo ya kusini.
Sasa ameolewa na ana watoto wawili huku akiishi kila siku kwa hofu kwamba mashushushu kutoka Kaskazini watamuua.

No comments: