SASA HAKULIKI - HAKULALIKI BAADA YA VITISHO VYA KOREA KASKAZINI...

Ramani ikionesha uwezo wa masafa ya makombora ya Korea Kaskazini. Pentagon imetangaza inasambaza mfumo wa kujilinda kwa makombora kwenye makao makuu ya jeshi la Marekani huko Guam na kujilinda kwa meli zenye makombora kwenye bahari kati ya Japan na taifa hilo jangili.
'Kunguru mwoga huepusha bawa lake'! Wananchi wa mji wa Kaesong, Korea Kaskazini wakikimbia mji huo kufuatia hatari ya kuzuka vita ya makombora ya nyuklia. 
Korea Kusini nako hali ni tete, ambapo maelfu ya wakazi wa huko wamekuwa wakikimbia makazi yao.
Majeshi ya Japan nayo yakiweka tayari vifaa vyao vya kijeshi tayari kwa lolote.

No comments: