BABU AFA KWA KUGONGWA NA GARI AKIMWOKOA SUNGURA BARABARANI...

Mtu mmoja amekufa kwa kugongwa na gari  wakati akijaribu kumwokoa sungura aliyejeruhiwa katika barabara ya njia mbili, doria ya Wyoming Highway ilisema jana.

William Kieren mwenye umri wa miaka 79 kutoka Laramie, alifariki Jumapili katika hospitali mjini Fort Collins. Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 3 usiku wa Jumamosi huko Wyoming 230, takribani maili sita magharibi mwa Laramie.
Askari mmoja alisema Kieren alikuwa amesimamisha gari lake kando ya barabara kuu hiyo na alikuwa karibu na mstari wa katikati ndipo akagongwa na gari lililokuwa likija kwa kasi.
Askari wa doria wamesema sungura huyo alikuwa angali hai katika barabara na hatimaye aliwekwa chini na askari mmoja.
Kwa mujibu wa ripoti, dereva aliyemgonga Kieren alikuwa mkazi mwingine wa Laramie,  Samantha Brown mwenye umri wa miaka 25.
Aliwaeleza maofisa kwamba aliona gari la Kieren liliwa limeegeshwa na akalazimika kuhamia upande mwingine ili aweze kulipita.
Samantha hakumwona mzee huyo kwenye barabara hadi alipogundua kwamba amegonga kitu fulani.
Mzee huyo mwenye miaka 79 alifariki dunia katika Kituo cha Afya cha Rockies huko Loveland, Colorado.
Mipango ya mazishi ya Kieren yanasubiria Kampuni inayoshughulika na mazishi ya Montgomery-Stryker Funeral Home.

No comments: