RAIS VLADIMIR PUTIN APITWA MSHAHARA NA MSEMAJI WAKE...

Rais Vladimir Putin (kushoto) na Msemaji wake, Dmitry Peskov.
Rais wa Urusi Vladimir Putin inasemekana alivuna Rubles milioni 5.7 (Pauni za Uingereza 119,000 )mwaka jana - lakini msemaji wake alivuna karibu mara mbili ya kiasi hicho.

Kwa mujibu wa msemaji wa Putin, Dmitry Peskov, alivuna Rubles milioni 11.1 (Pauni za Uingereza 233,000) katika mwaka uliopita - Rubles milioni 5.4 zaidi ya zile za Rais Putin.
Kuanika mapato ni sharti jipya kwa maofisa wa Urusi, ambalo lilianzishwa mwaka 2012.
Uanikaji huo umekuwa lazima kwa maofisa wa ikulu baada ya mshahara wa Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu Igor Shuvalov kupanda kwa kushangaza.
Katika moja ya uanikaji mishahara wa hivi karibuni kabisa, Shuvalov, msemaji huyo wa serikali kuhusu uchumi, alikuwa ndiye anayelipwa kiasi cha juu zaidi, akiwa na mapato ya familia ya Rubles milioni 449.4 (Pauni za Uingereza milioni 9.4).
Mshahara wake wa juu ulikuwa takribani nusu ya ule aliovuna mkewe, kwa mujibu wa tovuti ya Kremlin.
Msemaji wa Shuvalov alisema utajiri rasmi ulikuwa ulitokana na kuhamisha mali zake kurejesha nchini Urusi kutoka kwenye akaunti na mifuko aliyokuwa akimiliki nchi za nje.
Uamuzi wake ulisukumwa na mabadiliko yajayo katika Sheria za Urusi kuwafungia maofisa kuwa na akaunti na mali nje ya nchi.
Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev alivuna Rubles milioni 5.8 (Pauni za Uingereza 122,000) kwa mujibu wa data za Kremlin, wakati mkewe hakuanika mapato yoyote.

No comments: