KIJANA ALIYEBAKA BINTI WA MIAKA 11 ALISHAWAHI KUBAKA MWINGINE KABLA...

KUSHOTO: Wapelelezi wakichunguza eneo la tukio. KULIA: Opemipo Jaji.
Kijana mmoja anayetuhumiwa kumbaka msichana mwenye miaka 11 kwenye bustani alimshambulia msichana mwingine mwanafunzi mwaka mmoja kabla, mahakama imeelezwa.

Opemipo Jaji, mwenye miaka 18, anatuhumiwa kuwa alimfuatilia msichana huyo mwenye miaka 11 wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kutoka shule ndani ya basi.
Alimfuatilia binti huyo na kumburuta kwenye bustani ya Jubilee, Enfield, kaskazini mwa London, ambako alimfanyia unyama wa ubakaji kwa masaa matatu mnamo Novemba, mwaka jana, mahakama ilielezwa.
Glovu zake zilishindiliwa mdomoni mwake na akavuliwa nguo zake na kufanyiwa shambulio hilo.
Mwendesha mashitaka Rosina Cottage, alisema mtoto huyo alipanda basi huko Enfield Town sambamba na rafiki yake majira ya Saa 10:30 jioni.
"Alikuwa na umri wa miaka 11 na alikuwa amevalia sare zake za shule," alisema Cottage.
"Aliingia kwenye basi na rafiki yake na walikuwa wakicheka na kuongea. Pia ndani ya basi hilo kulikuwa na kijana wa kiume, mshitakiwa. Alimwona binti huyo akiteremka kutoka kwenye basi na kuanza kumfuatilia.
"Alimburuta kuelekea kwenye bustani eneo hilo gizani na kumbaka. Binti huyo alikimbia kwenda nyumbani huku akichuruzika damu na majeraha. Damu yake na kipimo cha DNA vilikutwa katika nguo za kijana huyo na kwenye begi."
Cottage alisema msichana huyo alikuwa akitarajiwa kufika nyumbani majira ya Saa 11 jioni na wazazi wake wakawapigia simu polisi majira ya Saa 11:30 jioni baada ya bimti yao kushindwa kurejea hadi muda huo.
Binti huyo alifika nyumbani Saa 2 usiku. "Alikuwa sio nadhifu, mchafu na mwenye mashaka.
"Alikuwa ameshikilia blauzi yake mkononi na kusema kwamba alikuwa ameshambuliwa."
Msichana huyo alisema mshambulizi wake 'aliendelea kumdunda ngumi na kukwea makonzi'.
Baadaye binti huyo aliieleza polisi kwamba baada ya kushuka kwenye basi hilo, aligundua mwanaume akitembea mbele yake na kisha nyuma yake. Alijaribu kumkwepa sababu alihisi kuna kitu hakikuwa sawa.
Katika bustani hiyo, alikuwa akitaka simu ya msichana huyo - ambayo hakuwanayo - kadi yake ya kusafiria na funguo zake.
Wakati fulani, alifikia kumtishia kumchoma visu endapo angeondoka na kumkamata alipojaribu kutaka kutoroka.
Pia alimtishia kumrekodi na kupeleka nakala kwa wanafunzi shuleni kwake, alisema binti huyo.
Msichana huyo alikimbilia nyumbani akiwa sio nadhifu, akibubujika damu na kufanyiwa upasuaji kutokana na majeraha yake.
Jaji, mkazi wa Edmonton, kaskazini mwa London, amekana kubaka na kusema hakuwa mshambulizi wa binti huyo, ingawa alikuwa ndani ya basi hilo.
Anadai vipimo vya DNA vya binti huyo kwenye begi lake, raba na ukanda wa nguo yake ya ndani vilitokana wakati alipokwenda kwenye bustani hiyo baadaye jioni ya siku hiyo, mahakama hiyo ya Old Bailey ilielezwa.
Lakini Cottage, akiendesha mashitaka, alisema 'haikuwa kufanana matukio' kwamba mnamo 2011, Jaji alipatikana na hatia ya shambulio la ubakaji na kumpora msichana mwingine aliyekuwa kavalia sare za shule.
Cottage alisema tai ilishindiliwa kwenye mdomo wa binti huyo, nguo zake zilivuliwa na alikuwa ameporwa simu yake na kubakwa.
Aliongeza: "Alikuwa akivutiwa na wasichana wanaoanza kukua na vitendo vya kutembea na visichana vinavyochipukia."
Kesi hiyo itaendelea leo.

No comments: