KIBAKA ANASWA AKIMWIBIA MTU SIMU KWA KUTUMIA VIJITI VYA KULIA CHAKULA...

Kibaka huyo akifanya vitu vyake mitaani mchana kweupe.
Mwizi mmoja wa mifukoni mjanja nchini China amenaswa kwenye kamera akiiba simu kwa kutumia fimbo mbili za kulia chakula.

Wang Hongbo, mwenye miaka 32, alinaswa akivuta simu kutoka katika mfuko wa mwanamke aliyekuwa akiendesha baiskeli maeneo ya Zhengzhou, mji mkuu wa jimbo la Henan katikati ya China.
Picha zinamuonesha akimkimbiza mwendesha baiskeli huyo ambaye hakuwa na habari kando ya barabara yenye pilika nyingi.
Akiwa kavalia koti la suti na suruali ya jeans, anaonekana akimfikia kwa kutumia fimbo zake mbili za kulia chakula na kwa umakini akiinua simu ya mwanamke huyo kutoka kwenye mfuko wake.
Mwizi huyo baadaye anaonekana akikagua mavuno yake hayo kabla ya kuuza simu hiyo, ambayo inadhaniwa kuwa iPhone, katika duka la karibu la vitu vilivyotumika.
Mpitanjia alimuona alipokuwa akiiba na kuanza kupiga picha tukio zima bila kificho. Baadaye akazituma picha hizo kwenye mtandao.
Shinikizo kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo baada ya picha zake kusambazwa kila kona, Hangbo akaonana na mwandishi wa habari wa eneo hilo, ambaye alirekodi habari yake na kumsindikiza pale alipokwenda kujisalimisha polisi.
Kwa mujibu wa Shanghaiist, tovuti ya maisha mjini Shanghai, Hangbo alirejea katika wizi sababu alikuwa akihangaika kumlea mtoto wake mwenye miaka 12 peke yake.
Hii si mara ya kwanza mwizi kuiba kwa kutumia fimbo za kulia chakula nchini China.
Mnamo Septemba 2011, wanaume wawili waliovalia makoti meusi walinaswa na kamera wakifanya doria kwenye mtaa mmoja kabla ya kuwanyemelea nyuma wateja waliokuwa wakifanya manunuzi wakiwa na chombo cha asili ya Kichina.
Wezi hao wasio na haya waliwatumia kwa umakini kuchomolea vitu vya thamani kutoka mifukoni mwa wateja hao waliokuwa hawajui chochote kinachoendelea.
Polisi nchini China ilisema magenge ya wezi wa mifukoni yalikuwa yakiwatumia kuwalenga wanunuzi wenye shughuli nyingi, hususani wanawake waliokuwa wameelemewa na mizigo mizito.
Mwenendo huo unadhaniwa kuwa unaenea kwa kasi kwenye miji mingi ya nchini China.
Wezi wa mifukoni wanafanya uhalifu huo kote nchini humo na wanapendelea hasa katika maeneo yenye pilika katika masoko ambako si rahisi kuhisiwa kutokana na msongamano mkubwa wa watu.

No comments: