HIVI NDIVYO KANUMBA ALIVYOTABIRI KIFO CHAKE...

  
Japo wengi wanasema kifo hakitabiriki, lakini hali ilikuwa tofauti kidogo kwa mwigizaji maarufu nchini Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012. Yeye siku chache kabla ya kufikwa na umauti, alifanikiwa kucheza filamu hii aliyoiita "LOVE & POWER" ambayo inaakisi sehemu kubwa ya matukio yaliyosababisha kifo chake. Leo jamii ya wapenda filamu, mashabiki wake na watanzania kwa ujumla tunaadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha Kanumba huku tukikumbuka umahiri wake wa kucheza na kamera. Katika kuadhimisha mwaka huo mmoja, kutakuwa na misa maalumu katika Kanisa la KKKT Kinondoni mida ya asubuhi ya leo. Kisha wote tutaelekea makuburi ya Kinondoni ambako mpendwa wetu amelala, na baada ya hapo tutaelekea Viwanja vya Leaders ambako tutajumuika kwenye uzinduzi rasmi wa filamu ya "LOVE & POWER" na familia ya marehemu itakabidhi tuzo kwa baadhi ya watu muhimu. Shughuli hiyo itasindikizwa na burudani kutoka bendi ya African Stars "Twanga Pepeta". Wote mnakaribishwa!!

No comments: