BABA AHOFIA MAISHA YA BINTI YAKE WA MIAKA MITANO ALIYEBAKWA...

Shambulio hilo limeibua hasira ya waandamanaji kote mjini Delhi.
Baba mzazi wa binti mwenye miaka mitano muathirika wa ubakaji amezungumzia hofu yake kwamba shambulio hilo la kikatili litamwacha binti huyo kutengwa na jamii kwa maisha yake yote yaliyobaki.

Kibarua huyo, mwenye miaka 32, alisema alihofia kwamba binti yake mdogo atajitenga na kilamtu sababu ya makovu yaliyozunguka shambulio la ubakaji katika nchi hiyo.
Alipata majeraha makubwa ndani ya mwili baada ya kuwa ametekwa, kubakwa na kuteswa mjini Delhi.
Kiongozi wa Chama cha Congress, Sonia Gandhi alimtembelea muathirika huyo mdogo hospitalini.
Shambulio hilo limetema cheche za maandamano ya hasira katika maeneo ambako yamefanya mwangwi wa kitendo kiovu cha ukatili mnamo Desemba kufuatia shambulio baya la ubakaji wa mwanafunzi mwenye miaka 23 ndani ya basi.
Baba wa binti huyo alihamia Delhi kutoka kijijini kwenye jimbo maskini kabisa nchini India, Bihar, miezi 18 iliyopita.
Alikuwa akijaribu kudunduliza fedha za kutosha kutoka kwenye ujira wake wa Pauni za Uingereza 2 kila siku aweze kurejea Bihar kujenga upya makazi yake, ambayo yalibomoka.
Alieleza: "Kamwe hatuwezi kurejea kijijini kwetu. Binti yangu hawezi kupata heshima au malezi anayohitaji.
"Hii itamfuata katika maisha yake yote. Kwa sasa hakika ninahofia kuhusu jinsi jamii itakavyomhukumu mwanangu na jinsi ya kumwezesha kupata elimu."
Binti huyo mdogo alitoweka wakati akicheza nje ya nyumba familia yake katika wilaya ya Gandhi Nagar jijini humo.
Mama yale alikwenda polisi. Hatahivyo, familia hiyo inasisitiza kwamba maofisa wa polisi hata hawakutoka kituoni hapo kwenda kusaidia - madai ambayo wamekanusha.
Binti huyo alipatikana siku tatu baadaye katika ghorofa ya chini baada ya majirani kugutushwa na kelele zake za kilio.
Wanaume wawili wanashitakiwa kwa kumbaka na kujaribu kumchinja koo lake.
Mashuhuda wanadai alikuwa ametapakaa damu na akiwa amekamata nguo yake katika hali ya kiwewe na kuishiwa maji.
Kitendo kiovu cha jamii kilichochewa na taarifa kwamba ofisa mmoja wa polisi alijaribu kuinunua familia hiyo ikae kimya.
Mfanyakazi huyo wa ujenzi alisema: "Watu kama hawa wanstahili kuuawa katikati ya mitaa kama mfano kwa wengine."
Ijumaa, binti mmoja wa miaka sita aligundulika akiwa amejeruhiwa vibaya kwenye vyoo vya jamii katika eneo la Badarpur, mjini Delhi.
Polisi wanahisi kwamba inawezekana alitelekezwa hapo baada ya kuwa amebakwa.
Muathirika huyo ametambuliwa kama mkazi wa mitaa ya ovyo karibu na Badarpur. Polisi wamewahoji takribani watuhumiwa 22 na kumshikilia mkandarasi wa choo hicho cha jamii.
Sekta ya utalii nchini India imeathirika na ongezeko la hivi karibuni la ripoti za ubakaji.

No comments: