AJIFUNIKA MFUKO WA PLASTIKI WAKATI NDEGE IKIPITA JUU YA MAKABURI...

Abiria wakimshangaa jamaa huyo aliyejifunika mfuko wa plastiki ndani ya ndege.
Si ajabu kwa watu kuwa na matambiko au miiko wakati wanaposafiri kwenye ndege, kama kuvaa mkufu wa Mt. Christopher au kuvumba macho yao hadi ndege inaporuka.

Lakini abiria mmoja alichukua imani zake hatua moja zaidi baada ya kujifunika kwa mfuko wa plastiki wakati wote wa safari yake sababu dini yake imemkataza kuruka juu ya makaburi.
Hili lilikuwa tukio la kituko lililowaacha hoi abiria wa ndege pale Myahudi wa Orthodox alipojifunika ndani ya mfuko wa plastiki.
Inaaminika mwanaume huyo ni wa Kohein, mfuasi wa dini ya mapadri wakongwe wa Israeli, ambao wanazuiwa kusafiri juu ya makaburi.
Picha hizo za ajabu, ambazo zimesambaa baada ya kuwa zimetumwa kwenye Reddit, zinaonesha abiria wenzake wakiwa wamenyanyuka kwenye viti vyao kuweza kushuhudia kituko hicho.
Sambamba na kuzingirwa na plastiki, mtu huyo alikuwa amevalia mavazi meusi, na kuonekana akiwa kavalia kibandiko cha Kiyahudi au 'kippah'.
Kama suluhisho lenye utata - si wote wanaruhusiwa na wote katika Orthodox ya Kiyahudi - mfuko wa plastiki unafanya kizuizi fulani kati ya Kohein na tumah wanaowazunguka, au najisi.
Kiongozi wa dini ya Kiyahudi (Rabbi), Jeffrey W. Goldwasser, wa hekalu la Beit HaYam nchini Israeli, alielezea: "Katika Orthodox na jamii zenye kushikilia ukale, Kohanim wanatarajiwa kuepuka kukutana na wafu, ambayo inahusisha katazo la kutembelea makaburi isipokuwa katika mazishi ya jamaa wa karibu."
Hata kama wanaweza kukingwa na mikanda ya viti, abiria hao hawatakuwa na uwezo wa kufikia maski ya oksijeni au kujiokoa upesi katika ndege wakati wa tukio la dharura.
Pia kuna swali la jinsi gani watakavyoweza kupumua.
Kutoboa matundu kabla katika plastiki inasemekana kubatilisha kizuizi hicho, kwa mujibu wa gazeti la Kiyahudi la YatedNe'eman.
"Endapo tu pale kohein anapovaa mfuko wake kwa bahati mbaya ukatoboka hapo kunaweza kuwa na huruma," ilidai makala hiyo.
"Kohanim wana kazi ya kulinda taharah yao, usafi," kwa mujibu wa makala hiyo.
Baadhi ya ndege zimechukua hatua zaidi na kuamua kupita njia maalumu kukwepa makaburi.
Na abiria wanaweza kufahamishwa kabla kama kuna mwili utakuwa ukisafirishwa katika ndege hiyo kwenye sehemu ya mizigo.
Picha hiyo iliyotumwa katika mtandao wa Reddit juzi, ilikuwa na maelezo yanayosomeka: "Myahudi wa Orthodox katika ndege pamoja na wanawake - hivyo kajifunika kwa kutumia mfuko wa plastiki..."
Mwaka 2001, Shirika la Ndege la El Al liliamua kutowaruhusu Wayahudi wa Orthodox kuvaa mifuko ya plastiki sababu 'taratibu za usalama wa kwenye ndege haziruhusu abiria kusafiri huku wakiwa wamejiziba kabisa kwa mifuko ya plastiki."
Mwaka mmoja baadaye ikaripotiwa kwamba mfanyakazi wa kwenye ndege aliingia katika majibizano na abiria ambaye alijaribu kusafiri huku akiwa kajifunika mfuko wa plastiki. Patashika hilo hatimaye likamlazimisha rubani kugeuza ndege na kurejea ilikotoka.
Mwanamke mmoja alifikia kumshitaki mfanyakazi wa ndani ya ndege kwa kumrudisha nyuma ya ndege pale mwanaume mfuasi wa Orthodox alipogoma kukaa pembeni ya mwanamke huyo.

No comments: