MWANAFUNZI ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME AKITOKA BAA...

Mwanafunzi kutoka Uingereza amebakwa na genge la wanaume wanne katika kibaraza nchini Thailand baada ya kuwa amekokotwa kutoka mtaani wakati akitoka katika baa mapema alfajiri.
Wanaume hao walikuwa wakirandaranda katika gari lao aina ya pick-up ndipo walipomwona msichana huyo mwenye miaka 20 akitoka nje ya baa hiyo maarufu ya usiku wa manane Jumamosi asubuhi.
Polisi walisema msichana huyo alikuwa amekunywa pombe na alikuwa ametelekezwa na msafiri mwenzake kutoka Afrika Kusini baada ya wote kuwa wameshauriwa kuondoka katika baa hiyo sababu ya hali zao.
Washambulizi hao walimkokotea kwenye kibaraza katika ghorofa ya pili ya jengo la jirani, ambako alikutwa Saa 11 alfajiri akitokwa machozi.
Muathirika huyo anadhaniwa kuwa ametokea Fort William, Invernesshire, na alikuwa ameshambuliwa jimbo la kusini mwa mjini mkuu la Nakorn Sri Thammarat.
Mwanafunzi huyo alikuwa ndio amewasili tu wiki mbili kabla na alikuwa akisubiri kusikia kama alikuwa amefanikiwa maombi yake ya kazi ya ualimu.
Mwanamke huyo mapema alikuwa kwenye Baa ya Rock 99 iliyoko Soko la Thawang kabla ya kuelekea mgahawa wa Nakorn Vientiane - mashuhuri kwa sababu inahudumia vinywaji katika muda wa ziada.
Polisi Luteni Kanali Niti Boonjan, mkuu wa uchunguzi alisema: "alikuwa ameomba kuwa mwalimu. Alikuwa bado akisubiria shule hiyo ijibu maombi yake ya kazi.
"Alikwaruzwa mwilini mwake na alipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi. Alikutwa akiwa analia katika kibaraza cha ghorofa ya pili."
Mwanamke huyo aliripotiwa kupigwa tumboni na washambulizi wake, aliowaelezea kuwa ni vijana, pale alipojaribu kukaidi matakwa yao.
Mkoa huo una wakazi wapatao 85,000 na uko maili 480 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo wa Bangkok.
Lakini eneo hilo liko mbali kutoka sehemu alipokuwa akielekea mtalii huyo hatahivyo, ikimaanisha fukwe hizo zilizoko kando ya ukanda wa pwani ya mashariki ya Ghuba ya Thailand zimebaki hazigusiki.
Nchi hiyo kwa ujumla, hatahivyo, inabaki kuwa mashuhuri kwa watalii wa Kiingereza - hasa wanafunzi - huku makumi elfu wakitembelea kila mwaka.

No comments: