MSANII AKON ATAKA TOVUTI, AAMBULIA DENI LA DOLA 127,000...

Jaribio la msanii Akon kutengeneza tovuti yake umeyeyushwa -- kwanza, tovuti hiyo umeota mbawa ... na sasa kampuni iliyokuwa ikifanya kazi hiyo inamshitaki kwa zaidi ya Dola za Marekani 127,000 ... imefahamika.
Atlanta Business Video hivi karibuni ilifungua kesi mjini Georgia -- ikidai ilikodishwa mwaka 2011 kuhariri video ya "Fantrace" lakini haikuwahi kulipwa hata senti moja.
Video ya "Fantrace" ilitengenezwa na Akon na washirika wawili wa kibiashara ambao walitaka iwekwe kwenye aina ya majadiliano kama ya Facebook ambako mashabiki wa watajibizana na mastaa. Wazo zuri, lakini kwa mujibu wa Atlanta Business Video halikutendewa haki.
Atlanta Business Video inasema ilitumia humo masaa 1,023 ya kazi -- yanayogharimu Dola za Marekani 127,875 -- na wanataka kulipwa.

No comments: