MKONGWE WA UTENGENEZAJI KATUNI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 91...

Bob Godfrey, mtengenezaji katuni mkongwe aliyefanikisha katuni bora za watoto za Roobarb & Custard na Henry's Cat, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91, familia yake imethibitisha jana.
Mzaliwa huyo wa Australia, ambaye amefurahia kazi yake kwa karne tano, ameshinda tuzo tatu za Baftas kwa kazi yake na pia Tuzo ya Oscar kutokana na filamu yake fupi ya Great, ambayo iliangazia maisha ya mhandisi Isambard Kingdom Brunel.
Katuni za paka na mbwa za Roobarb zilihadithiwa na  Richard Briers, ambaye alifariki Jumapili iliyopita akiwa na miaka 79, na zilipata umaarufu mkubwa mno kwa mada zake zilizokamata na uhuishaji wake.
Godfrey alianza maisha yake ya kazi kama mchoraji kabla ya kujiunga na studio ya ubunifu na kuingia kwenye utengenezaji katuni. Kazi yake ya mwisho ilikuwa Millennium: Muziki kwa ajili ya Channel 4 mwaka 1999.
Mtengenezaji katuni huyo, ambaye alipata elimu yake mashariki mwa Londoni, alibainisha mwaka 2001 kwamba alikuwa na jutio moja, akisema: "Nilipendelea kuwa nimefanya makala moja kamili lakini siwezi kuonekana kujirefusha mwenyewe kwa urefu huo.
"Pale unapotazama filamu zangu, zinaonekana kuwa mfululizo wa matangazo ya biashara ya sekunde 30 kwa pamoja," alilieleza gazeti la The Guardian.
"Mimi ni mtu wa umbali mfupi nitake au nisitake."
Mwanzilishi wa Studio ya Aardman Animations, Peter Lord alisema kwenye mtandao wa Twitter: "Mpendwa mzee Bob Godfrey hatunaye tena."

No comments: