Stephen Wassira. |
Serikali inatarajia kuajiri walimu 25,000 wa sekondari mwakani ili kupunguza uhaba wa walimu katika shule za sekondari za Serikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, alisema hayo juzi wakati akihutubia mikutano ya hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti wilayani humu.
Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini ikiwemo upungufu wa walimu ambao sasa umegeuka kuwa mzigo kwa wazazi na walezi ambao wanachanga fedha za kuwalipia mishahara walimu wa kujitolea wanaofundisha shule hizo.
Alisema mbali na kuwapunguzia mzigo huo wazazi, Serikali pia itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa shule hizo ikiwa ni pamoja na kujenga hosteli na kuweka huduma za maji na umeme hasa kwa shule za vijijini ili walimu na
wanafunzi wapate huduma hizo kwa urahisi.
“Tutaongeza walimu na kuboresha mazingira ya elimu. Januari mwakani walimu 25,000 wa Shule za Sekondari wataajiriwa na kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu mashuleni,” alisema Wasira.
Kuhusu madai mbalimbali ya walimu, Wasira alisema Serikali inayatambua na kuyafanyia kazi kwa kuwa ni watu muhimu katika kuboresha elimu nchini.
Alikiri kwamba Serikali ilichelewa kuyatatua baadhi ya madai hayo kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya uchumi na kusema hata hivyo inaendelea kuyatatua kadiri hali inaporuhusu.
Katika hatua nyingine, Wasira aliwasisitizia umuhimu wa wazazi na walezi kuwasomesha watoto wao bila ubaguzi akisema elimu haina mbadala maishani huku akiwataka wajenge uhusiano mzuri na walimu katika kufuatilia na kusimamia maendeleo ya watoto wao na kukuza taaluma ya mtoto.

No comments:
Post a Comment