Mmoja wa wanaharakati akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa binti huyo aliyebakwa na wahuni. |
Kundi la wahuni lililomshambulia msichana wa India ambaye baadaye alifariki kutokana na majeraha yake ya kutisha walijaribu kumkanyaga na basi hilo alimobakwa, imebainika jana.
Msichana huyo mwenye miaka 23 alitoswa nje ya basi hilo lililokuwa katika mwendo ambapo aliokolewa na mchumba wake ambaye alimvuta kutoka chini ya magurudumu ya basi hilo, polisi mjini Delhi wamesema.
"Walijaribu kulielekeza basi alikoangukia binti huyo na rafiki yake wa kiume. Rafiki yake akamvutia msichana huyo sehemu iliyo salama, kwa wakati muafaka", ofisa ambaye yuko karibu na uchunguzi amedai.
Majirani walisema wawili hao walikuwa wamepanga kufunga ndoa Februari mwaka huu lakini msichana, ambaye bado hajafahamika, alifariki Jumamosi iliyopita licha ya matibabu katika hospitali nchini Singapore - wiki mbili baada ya kushambuliwa.
Waziri Shashi Tharoor alisema endapo wazazi wake hawatakuwa na pingamizi basi atatajwa hadharani majina yake.
Nchini India waathirika wa ubakaji hawatajwi majina yao kwa namna yoyote ile chini ya kifungu 228-A cha Kanuni ya Adhabu.
Imefahamika juzi kwamba msichana huyo aliieleza familia yake kabla ya kukata roho kitandani kuwa alijitahidi kadri ya uwezo wake kupigana na wabakaji hao wamwachie.
Msichana huyo alimweleza kaka yake kwamba aliwapiga mateke wanaume hao wakati wakimbaka ndani ya basi mjini Delhi. Wakati wakimbaka mwanafunzi huyo, wanaume hao walisema wangemuua.
Kufuatia kifo chake kaka yake ametoa heshima za mwisho kwa ujasiri na hamasa aliyoonesha kufuatia mateso yake hayo.
Alisema: "Alikuwa na nguvu mno. Mara zote alisema mtu hawezi kuvumilia mateso ila kupambana nayo.
"Wakati alipolazwa hospitalini, alinieleza kwamba alipambana mno kadri alivyoweza. Alikuwa akijilinda kwa kuwapiga na kuwang'ata.
"Aliwasukuma na kuwapiga mateke pia. Walichemka kwa hasira kutokana na kujilinda kwake hivyo wakaamua kumuua. Alinieleza kwamba walikuwa wakibwabwaja 'maar do ise' (muue). Walimtupa nje wakidhani kwamba alikuwa amekufa."
Katika mahojiano na gazeti la The Indian Express jana, kaka huyo alisema yeye na familia wanaamini kwamba angeweza kunusurika kifo endapo angekimbizwa mapema nchini Singapore kwa matibabu ya kuokoa maisha yake.
Alisema dada yake alipatwa na mfululizo wa maambukizi yanayoepukika mjini Delhi.
Mwanafunzi huyo alisafirishwa kwenda Hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore siku tano zilizopita - takribani wiki mbili baada ya kuwa amebakwa na kundi la wahuni sita ndani ya basi mjini Delhi.
"Pengine wangekuwa wameweza kumwokoa, lakini uamuzi huo ulichelewa," alisema kaka yake, akiongeza: "Hospitali ya Mount Elizabeth ina viwango vya juu mno vya usafi. Wangeweza kumkinga na maambukizi hayo."
Tukio hilo limekuja huku muathirika wa pili, msichana wa miaka 16 anadai alibakwa na kondakta katika basi mjini Delhi siku hiyo hiyo ambayo muathirika aliyebakwa na wahuni alipofariki.
Mwili wa msichana huyo wa miaka 23 ulichomwa juzi baada ya kuwa umerejeshwa mjini Delhi kwa ndege iliyokodiwa na Serikali ya India.

No comments:
Post a Comment