Paroko Ambrose Mkenda. |
Polisi Zanzibar inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi Paroko Amrose Mkenda (52) mwishoni mwa wiki iliyopita.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, ACP Yusuf Ilembo, alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana kwa ushirikiano wa Polisi Zanzibar na makachero waliotoka Makao Makuu, Dar es Salaam.
Hata hivyo, alikataa kuwataja watuhumiwa hao kwa madai ya kuhofia kuingilia upelelezi wa kuwapata wengine.
Alisema watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa ili kuwapata washiriki wenzao waliopanga njama pamoja za kumvamia na kumjeruhi kwa risasi Paroko Mkenda wa Parokia ya Mpendae mjini Zanzibar.
Ilembo alisema Polisi itahakikisha wale wote waliohusika na shambulio hilo wanatiwa nguvuni na kukabiliana na mkono wa Sheria.
No comments:
Post a Comment