Padri Ambros Mkenda akiwa kitandani hospitalini. |
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae, Ambos Mkenda, amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi sehemu za shingo na mdomoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo pamoja na kuwatia mikononi wahusika.
“Tumeanza kufanya uchunguzi kuweza kujua watu waliohusika na tukio hilo ambapo kwa sasa ni mapema sana kutoa taarifa ya tukio hilo,” alisema Kamanda Juma.
Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa wakiendesha pikipiki aina ya Vespa katika maeneo ya Tomondo nje kidogo ya mji wa Unguja, saa moja usiku juzi.
Inadaiwa kuwa waliotenda uhalifu huo walikuwa wakimfuatilia wakidhani kwamba alikuwa na fedha zinazotokana na michango iliyokusanywa na waumini katika ibada ya Krismasi kanisani hapo.
“Zipo taarifa tofauti, kuna dhana kwamba Padri Mkenda alikuwa na fedha za michango kanisani kwa hiyo watu hao walikuwa wanataka kumpora,” alisema mmoja ya watu waliokuwa pamoja na padri huyo.
Hata hivyo, watu hao baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya Padri Mkenda, waliendelea na safari zao bila ya kufanya uvamizi na upekuzi katika gari alilokuwa akitumia padri huyo.
Imeelezwa kwamba padri huyo amejeruhiwa vibaya katika sehemu za shingo pamoja na mdomo, na amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Awali, baada ya tukio, padre huyo alifikishwa katika Hospitali binafsi ya Al-Rahma iliyopo Kilimani, lakini kutokana na majeraha makubwa aliyo nayo alilazimika kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
Waumini wa Parokia ya Mpendae walifurika kwa wingi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mara baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi kwa kiongozi wao kwa ajili ya kufuatilia taarifa za matibabu yake.
Daktari mmoja anayemshughulikia kwa karibu Padri Mkenda, alisema amejeruhiwa vibaya sehemu za shingo na mdomo, hali iliyosababisha apoteze damu nyingi.
Alisema alipofikishwa hospitalini hapo kazi kubwa ya kwanza iliyofanywa ni kutoa risasi mbili katika mwili wake.
“Kwa sasa tunajaribu kuzuia kupoteza damu nyingi ambayo inatokana na majeraha makubwa aliyoyapata,” alisema daktari huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.
Askofu wa Jimbo la Zanzibar, Agustino Shao, alikiri kutokea kwa shambulio hilo dhidi ya Padri Mkenda na kwamba kutokana na hali yake amepewa rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Alisema jimbo halijui ni nani aliyefanya shambulio hilo, lakini walipata taarifa kuwa vijana wawili waliokuwa katika pikipiki walishuka na kumfuata padri kwenye gari na kutekeleza unyama huo. Waliliripoti Polisi na Polisi wanaendelea na uchunguzi.

No comments:
Post a Comment