MWANAMKE AAMBIWA AKATOLEWE INZI, AKAISHIA KUBAKWA MOROGORO...

Kamanda wa Polisi, Faustine Shilogile.
Polisi mkoani Morogoro inamsaka mtu aliyembaka mwanamke baada ya kudai kwamba amemeza nzi na kwamba atapata matatizo makubwa iwapo hatamtoa mdudu huyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, kuwa tukio hilo ni la Oktoba 30 jioni katika  maeneo ya Mazimbu mkoani hapa.
 Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikutana na mwanamke huyo na  kumlaghai hivyo na kumtaka waende vichakani ili amtapishe  na kwamba baada ya kufanyiwa tendo hilo mtu huyo akatokomea kusikojulikana.
Kamanda huyo alisema kuwa mtu huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake hajakamatwa na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Hata hivyo, kamanda  alihadharisha jamii dhidi ya  matapeli wenye tabia hizo ambao polisi  inawachunguza watiwe mbaroni.
Wakati huo huo  Mohamed  Juma amefariki dunia baada ya kudondoshwa na dereva wa bodaboda ambaye alitoweka   na kumwacha akiwa na majeraha makubwa sehemu za kichwani.
Kamanda huyo alisema watu wawili Aziz Zuber na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Amani  walimkuta mtu huyo akiwa na hali mbaya barabarani katika eneo la Kinole.
Walimchukua na kumpeleka hospitali ya mkoa.  Alisema kuwa wakati watu hao wakifuatilia karatasi ya kutibiwa ya polisi PF 3, waliporudi hospitalini walikuta majeruhi huyo amefariki.

No comments: