MTOTO WA MIAKA MIWILI AUAWA NA MBWAMWITU KWENYE BUSTANI YA WANYAMA...

Mtoto wa kiume mwenye miaka miwili ameng'atwa hadi kufa na mbwamwitu wenye njaa kali wakati alipodondoka kutoka sehemu aliposimamishwa na mama yake kwa ajili ya kuwatazama wanyama hao kwenye bustani ya wanyama ya Pittsburgh na Tangi la Samaki.
Waokoaji waliokata tamaa wakisaidiwa na walinzi wa bustani hiyo pamoja na askari polisi wenye silaha walijaribu kuwashusha makali wanyama hao wenye uchu wakati wakimshambulia vikali mtoto huyo, kutoka Pleasant Hills, mjini Pittsburgh, Jumapili asubuhi.
Walinzi wa bustani hiyo walifyatua vishale na maofisa polisi wakafyatua risasi, na kuua mmoja wa mbwamwitu hao, mnyama hatari zaidi, lakini waokoaji bado hawakuweza kumfikia mtoto huyo kwa wakati muafaka.
Gazeti la Pittsburgh Post limeripoti kwamba mtoto huyo alianguka kutoka alipokuwa na kupenya kwenye wavu ambamo mbwamwitu walikuwa wakioneshwa majira ya saa 5:45 asubuhi ya Jumapili.
Mama yake aliyejawa na woga, mwenye miaka 34, ambaye alimpeleka mtoto huyo kwenye bustani, alishuhudia wakati mbwa hao wakimshambulia mtoto wake.
Polisi hawafahamu kama mtoto huyo alikufa kutokana na kuanguka kutoka katika wavu huo wenye urefu wa futi 11 au kufuatia shambulio hilo.
Luteni Kevin Kraus kutoka polisi wa Pittsburgh ameelezea tukio hilo kuwa ni ya 'kuogofya.'
"Kwa bahati mbaya, mbwa hao walielekeza akili zao kwenye shambulio na si kufuata maelekezo ya walinzi wa bustani hiyo kujaribu kuwadhibiti," uongozi wa bustani hiyo ulisema katika taarifa yake.
Walinzi wa bustani hiyo kwa haraka wakafanikiwa kuwatimua mbwamwitu saba, ambao walikuwa wadogo kidogo kuliko Labrador, lakini wengine hawakuweza kuzuilika.
Wafanyakazi walivuka wavu huo na kuwapigia kelele wanyama hao katika juhudi za kuwazuia. Mvua ya vishale pia haikufanikiwa kuwarudisha nyuma wanyama hao.
Pale polisi wa Pittsburgh walipoingilia kati, hasa mbwa mmojawapo alipunguzwa kasi na kuacha kumshambulia mtoto huyo. Alikuwa kapigwa risasi na ofisa mmoja wa polisi.
Maofisa wa bustani hiyo ya wanyama walisema kuna wavu mbele ya sehemu ya kusimamia, lakini Luteni Kraus alisema ulitengenezwa kwa ajili ya kunasa vitu vidogo kama kamera, na sio binadamu.
Wachunguzi hawakusema sababu hasa za kifo, alisema.
Ofisi ya Mkemia ya Allegheny County alisema jina la mtoto huyo halitawekwa hadharani hadi baadaye leo (Jumapili).
Mtoto huyo na mama yake walikuwa wakitembelea bustani hiyo pamoja na jamaa zao - mtu mzima na mtoto mwingine - wakati wa shambulio hilo.
Polisi walisema baba wa mtoto huyo aliwasili mapema baasa ya tukio hilo na kwamba wazazi hao wote wawili wanapatiwa matibabu kufuatia mshituko waliopata.
Bustani hiyo ilifungwa, na haikufahamika mara moja lini hasa itafunguliwa tena, mamlaka zimesema.
"Kelele ziliendelea kusikika kutoka kila upande: "Msaada. Tusaidieni jamani," shuhuda Angela Ciniti mwenye miaka 20, ambaye alitembelea bustani hiyo akiwa na rafiki yake wa kiume amelieleza Gazeti la Pittsburgh-Post.
"Tulikuwa njiani kwenda kutazama dubu ndipo tukasikia kelele kali za kuomba msaada," anakumbuka Ciniti. "Mtu fulani alikuwa akiomba msaada, akiomba mtu yeyote asaidie."
Wamekuwa maarufu kwa kuua kongoni na pundamilia, ingawa kwa kawaida wamekuwa wakishambulia wanyama wasiokuwa na hatari.
Mbwa hao, ambao ni hatari, ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi kwatika Uwanda wa Serengeti.
Katika mawindo yao huishia kufanikiwa kuua asilimia 80 kwa wakati mmoja. Simba hufanikiwa kuua kiwango cha asilimia 30 pekee.

No comments: