'DOGO' MKALI WA FILAMU YA "KARATE KID" ATIMIZA MIAKA 50!...

KUSHOTO: Ralph Macchio alivyo sasa. KULIA: Ralph akiwa na Pat Morita 'Mr. Miyagi' (kulis) katika filamu ya Karate Kid.
Yule dogo mkali wa filamu ya "Karate Kid", Ralph Macchio sasa ana umri wa miaka 50!
Ni ngumu kuamini, lakini Ralph amesherehekea kutimiza miaka hiyo jana, ikiwa ni miaka 28 tangu filamu hiyo ilipoingia mtaani kwa mara ya kwanza.
Alizaliwa Novemba 4, 1961 na kwamba alicheza filamu ya "Karate Kid I" mwaka 1984 (akiwa na miaka 23) na "Karate Kid II" mwaka 1986 (akiwa miaka 25).
Na kwa kipindi chote hicho tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo aliyocheza kama Daniel-san, Ralph amekuwa mvulana aliye bize mno.
Baada ya kuongoza katika "The Karate Kid" na filamu tatu zilizofuatia katika mfululizo wa filamu hiyo, Macchio aliendelea kufanya kazi katika filamu, akifanya muziki katika Broadway, akiigiza kwenye televisheni na siku za hivi karibuni kabisa alionekana kwenye "Dancing with the Stars."
Lakini wapi mfululizo wa filamu hizo ulipoishia?
Jambo la kuhuzunisha ni kwamba, Pat Morita (Mr. Miyagi) alifariki mwaka 2005, lakini nyota wengine waliocheza kwenye mfululizo wa filamu hiyo wamekuwa na mafanikio makubwa, huku wakitamba kwenye shoo kama "Glee" na "Mad Men" na wamechaguliwa kwenye Tuzo za Oscar na kushinda.

No comments: