MJASIRIAMALI BILIONEA KIZMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MSICHANA UFUKWENI...

KUSHOTO: Bilionea Greg Cox. KULIA: Ufukwe wa Bondi ambao Cox anadaiwa kufanya shambulio la ubakaji katika maeneo la jirani na hapo.
Bilionea kijana wa zamani wa shule za jamii amepandishwa kizimbani nchini Australia kwa madai ya kubaka msichana mdogo kwenye ufukwe wa Bondi.
Mjasiriamali huyo Greg Cox mwenye miaka 32, anatuhumiwa kwa shambulio la ngono dhidi ya msichana wa miaka 21 anayetoka Bermuda katika baa moja iliyoko kwenye ufukwe huo Januari mwaka huu.
Cox, mkazi wa Battetsea, South London, hakukanusha kufanya mapenzi na msichana huyo lakini alisisitiza kwamba wote walishiriki kikamilifu tendo hilo.
Akisimama mahakamani Septemba, wanasheria wake waliweka pingamizi bila mafanikio kuzuia jina lake lisiandikwe kwenye vyombo vya habari kujaribu kulinda rekodi yake nzuri ya nyuma na mafanikio yake katika shughuli zake.
Walijenga hoja kwamba ukweli kuwa ametoka katika familia inayofahamika sana na kuhudhuria shule ya bweni - Millfield karibu na Glastonbury, Somerset - sambamba na kuibuka katika jamii ya wafanyabiashara wa Uingereza, angeweza kuathirika na 'usumbufu asiostahili' kutokana na mashitaka hayo.
Katika kikao cha jana cha usikilizwaji hatia, kilichokaa kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha kumshitaki, Wakili wa Cox, Graham Turnbul, alisema kulikuwa na 'kutofautiana' katika taarifa za matukio ambazo mdaiwa kuathirika amekabidhi polisi.
Alidai kuwa, uchunguzi wa kina wa madai yake unaweza kufumbua na kulikuwa na nafasi ya kutosha mashitaka dhidi ya Cox yangeweza kutupiliwa mbali.
Kama haitoshi, Hakimu Greg Walsh aliamua 'kesi haiwezi kuwa bila ushahidi thabiti' na nafasi ya Cox kushitakiwa kwa haki isingeweza kufanyiwa upendeleo.
Mfanyabiashara huyo - ambaye anaendesha kampuni ya kutoa mikopo kwa wateja wenye mitaji midogo - anatumia muda wake mwingi kuzunguka duniani kwa starehe au mikutano ya kujitangaza kibiashara.
Katika miaka ya hivi karibuni amekuwa mkurugenzi katika makampuni kadhaa na alikuwa akiishi kwenye ghorofa lenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni moja lililoko Battersea, huko South London.
Anasemekana alikutana na msichana huyo anayetuhumiwa kumbaka katika klabu ya usiku ya Bucket List iliyoko karibu kabisa na Bondi.
Shambulio hilo inadaiwa lilitokea Januari 22 kati ya Saa 5:10 na Saa 5:30 usiku. Cox amekana madai yote dhidi yake.
Kwa mujibu wa Gazeti la Sunday Telegraph la mjini Sydney, Cox amekuwa akiishi kwenye nyumba za kifahari zilizoko ufukweni katika kitongoji cha Bronte, maili chache kutoka Bondi.
Anasemekana kuwa amekuwa akipunga upepo kwenye kisiwa cha Hamilton, nje ya Pwani ya Queensland, na kuhudhuria matukio ya michezo ya kuelea baharini kwenye kitongoji cha Manly mjini Sydney.
Wanasheria wake jana wameomba kurekebisha masharti kwa ajili ya dhamana yake ili kumwezesha kurejea Uingereza kutazama fursa za biashara yake.
Lakini hakimu ameamua kwamba ni juu ya Mahakama ya Wilaya kuamua kama Cox aruhusiwe kurejea nyumbani kabla ya kesi, ambayo kuna uwezekano kufanyika kabla ya Mei, mwakani.
Kwenye mtandao wa kampuni ya Quintessential, ameelezewa kama mjasiriamali mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 akiendesha kampuni yake mwenyewe 'tangu mwanzo hadi kufikia mapato ya Pauni za Uingereza milioni 40'.
Imeelezwa Cox na wenzake walikuwa Sydney kuhudhuria mkutano wa masoko ya digitali uliofanyika kwenye ukumbi wa Darling Harbour, Januari mwaka huu.
Malengo yake, Cox amesema katika ukurasa wake binafsi wa tovuti, kwamba 'rahisi mno - kuwa bora katika kila nifanyacho'.
Pia anamiliki kampuni yenye makao yake London inayoitwa Cloud9 Media.
Kampuni yake ya Quintessential Finance imejijengea heshima kubwa katika mahusiano na washirika wake wa kibiashara, ikitoa mialiko kusherehekea mjini Las Vegas na kuwasiliana kupitia mtandao wa Twitter.

No comments: