Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, kupinga uamuzi wa kusitisha mgomo uliotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, kwa madai ulikuwa batili.
Katika rufaa hiyo iliyowasilishwa juzi mahakamani hapo na Wakili wake, Gabriel Mnyele, CWT inadai kuwa uamuzi huo uliotolewa na Jaji Sophia Wambura haukufuata sheria.
Mnyele anadai Jaji alikosea kisheria kuamuru mgomo huo usitishwe kwa madai ulikuwa batili na pia alikosea kisheria kuamuru taarifa ya kwanza ya kuzuia mgomo ilikuwa mbaya kisheria kwa sababu ilitolewa siku za mwisho wa wiki.
Jaji Wambura pia anadaiwa kukosea kuamuru kwamba mgomo ulipaswa kuwa na kikomo na alikosea kusema upigaji kura wa wanachama wa kuunga mkono haukufanyika kihalali.
Katika hati hiyo ya kukata rufaa, Mnyele alidai Jaji Wambura alikosea kisheria kuwaamuru wakata rufaa kulipa fidia bila uthibitisho.
Katika uamuzi huo unaokatiwa rufaa, Jaji Wambura aliamuru chama hicho kusitisha mgomo, kulipa hasara kwa wanafunzi iliyosababishwa na mgomo huo, ikiwa ni pamoja na kufidia muda wa masomo waliyokosa wakati wa mgomo.
Jaji Wambura alisema sheria ilikiukwa na chama hicho kutoa notisi ya siku 48 Ijumaa na kuanza mgomo Jumatatu asubuhi, huku wakijua siku za mwisho wa wiki hakuna kazi serikalini.
Aidha, alisema walitangaza mgomo wakati kesi ikiwa mahakamani, hivyo pamoja na kuwapo upigaji kura kwa wanachama wake kukubali au kukataa mgomo huo, bado haikuwa sahihi. Alisema pia kulikuwa na kasoro, kwa kuwa hawakueleza kisheria ni mgomo wa aina gani na ukomo wake.

No comments:
Post a Comment