NELLY AONGELEA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA KWENYE BASI LAO...

Mwimbaji Nelly amezungumza hadharani kuhusu kukutwa dawa za kulevya kwenye basi lake analotumia katika ziara, akisema hakukuwa na dalili zozote kwamba gari hilo lilikuwa limepakia heroin na bangi.
Nelly alieleza, "Ninaelewa mmoja wa wafanyakazi wangu alifanya uamuzi usio wa busara kupakia vitu vinavyokatazwa kisheria ndani ya basi na kusababisha kukamatwa kwake jana asubuhi.
Kama ilivyoripotiwa awali, Polisi huko Sierra Blanca, mjini Texas wamesema walikuta kete 36 za heroin, zaidi ya kilo 10 za bangi, na bastola. Imeelezwa abiria mmoja ndani ya basi, Brian Keith Jones, alikamatwa baada ya kukiri kwamba dawa hizo na silaha ni vyake.
Nelly aliongeza, "Si mimi wala yeyote mwingine katika basi alikuwa akijua uamuzi wake wa kupakia vitu hivyo kwenye basi. Maofisa wa vyanzo vya kisheria hawakufungua mashitaka yoyote shidi ya yeyote mwingine zaidi ya mtu huyo."
Vyanzo vya kisheria vimesema uchunguzi wa dawa hizo kwenye kete umethibitisha ilikuwa heroin - lakini vyanzo vilivyo karibu na Nelly vimedai ilikuwa Molly ama maarufu kama 'kirusha akili halisi'.

No comments: