MTANGAZAJI NA MWIGIZAJI MKONGWE AFARIKI DUNIA...

Mwendesha vipindi vya televisheni na mwigizaji mkongwe, Gary Collins amefariki dunia jana mjini Biloxi akiwa na umri wa miaka 74.
Taarifa zimesema alifariki kutokana na sababu za kawaida kabla ya saa 7:00 usiku wa manane katika Kituo cha Afya cha Mkoa mjini Biloxi.
Kabla ya kifo chake, Collins aliwahi kuonekana kwenye shoo zilizotikisa kama "Fantasy Island", Charlie's Angels", "Alice", "The Love Boat", "Police Story", na nyingine nyingi sana.
Collins pia alipata umaarufu kupitia kipindi chake cha televisheni cha "Hour Magazine" na kutoka mwaka 1980 hadi 1988 na kuendesha Shindano la Urembo la Miss America kuanzia mwaka 1985 hadi 1989.
Alimuoa Mrembo wa zamani wa Marekani, Mary Ann Mobley mwaka 1967 na wawili hao kufanikiwa kupata mtoto mmoja. Walitalikiana mwaka jana.
Collins pia alikuwa na watoto wawili aliowapata katika ndoa yake iliyopita hapo kabla.
Katika miaka michache iliyopita, Collins alikumbwa na mizozo kadhaa ya kisheria, ikiwamo ya kukamatwa akiendesha gari huku akiwa amekunywa pombe kuzidi kiwango.

No comments: