MAMA WA SAGE STALLONE ATAKA KURITHI MALI ZOTE...

Marehemu Sage Stallone.
Mama we Sage Stallone amemtaka Jaji kumruhusu asimamie mali za kijana wake huyo ambazo zina thamani ya Dola za Marekani 40,000 (Zaidi ya Shilingi milioni 63).
Sasha Madron anadai Sage alifariki bila kuacha wosia wowote, na kwamba ameacha mali zenye thamani ya Dola 40,000.
Sasha anataka mamlaka kamili yatakayomwezesha kuwa na maamuzi yote kuhusu mali hizo.
Sage alifariki dunia Julai, mwaka huu. Mkemia Mkuu alisema Sage alifariki kutokana na mshituko wa moyo, na sio matumizi ya dawa za kulevya. 
Hakuna dawa zozote zilizogundulika kwenye mfumo wake wa damu wakati wa kifo chake.

No comments: