KIBABU CHAKABWA NA KUKOMBWA PESA ZOTE KWENYE AKAUNTI...

KUSHOTO: Supamaketi ambako shambulio lilitokea. KULIA: Michael Saxby.
Mzee mkongwe wa vita jana amewashutumu wanunuzi kwa kudharau kilio chake cha kuomba msaada wakati alipodhibitiwa ndani ya gari lake na majambazi kwenye maegesho ya magari yaliyo kwenye mtaa wa supamaketi wenye pilika nyingi mchana kweupe.
Michael Saxby mwenye miaka 83, alisema alikuwa akipiga kelele kuomba msaada huku mwanamke na mwanaume wakimvamia nje ya duka lake la Tesco na kisha majambazi kufanikiwa kutokomea na akiba ya maisha ya wastani.
Hakuna yeyote aliyethubutu kukimbilia kutoa msaada kwa mstaafu huyo ambaye anaweza kutembea tu kwa msaada wa magongo - licha ya kwamba shambulio hilo limetokea hatua 20 tu kutoka lango kuu la supamaketi majira ya saa 5:30 asubuhi siku ya Ijumaa iliyokuwa na pilika nyingi.
Mzee Saxby ambaye anatokea Cottenham, huko Cambridgeshire, anaamini wezi hao walimrekodi kwa kutumia simu ya mkononi wakati akiingiza namba ya siri sehemu ya kutokea kwenye supamaketi hiyo.
Baadaye walimvamia na kumwibia pochi yake ya mfukoni na kupukutisha akiba yake yote iliyokuwa na Pauni za Uingereza 700 (karibu Shilingi 1,750,000) alizokuwa akitegemea kutokana na malipo yake ya pensheni.
Babu huyo, ambaye miguu yake ilijeruhiwa katika miaka ya 1950 kutokana na mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini, alisema jana amesikitishwa mno na wote walioshindwa kumsaidia.
Alisema: "Nilikwenda kwenye gari langu takribani nafasi sita kutoka lango kuu ndipo mwanaume huyu akachomoa pochi yangu kutoka mfukoni na kisha kunikandamizia kwenye gari langu.
"Alinikandamiza kifuani kwa goti lake na nilipojaribu kujitetea, mwanamke akaninyakua kifundo na kupora pochi yangu na kuchukua kadi zangu za benki.
"Kilichonipa ghadhabu na kunisikitisha ni kuwa nilikuwa nikipiga kelele za kuomba msaada kwa sauti yangu ya juu kabisa na kulikuwa na watu kama kumi waliokuwa jirani na hapo ambao walinipita bila kunisaidia.
"Mara msichana mmoja akaanza kutufuata pale lakini mwanamke jambazi akaoneshea kidole kichwani kwake kumpa ishara kwamba mimi ni kichaa, na msichana yule akaendelea na safari yake."
Mjane, ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye Hospitali ya Addenbrooke’s kwa miaka 43 na kutunukiwa na taasisi ya Royal Humane Society mwaka 1942 kwa kumwokoa kijana aliyekuwa akizama kwenye mto, anaamini wezi hao walimfuatilia wakati alipokuwa akiingia ndani ya duka hilo.
Mzee Saxby alisema: "Nilimwona mwanamke ambaye alinyakua pochi yangu kwenye mgahawa uliomo katika supamaketi hiyo.
"Alikuwa akiongea na simu kila wakati ambapo mtu mzee alipokuwa akiingia. Naamini alikuwa akiturekodi tulipokuwa tukiingiza namba za siri."
Polisi wanaowasaka wahalifu hao jana waliwaelezea kuwa wote huvaa nguo nyeusi. Mwanaume ana muonekano wa Kimediterranea na kwamba ana umri kati ua miaka 23-24, wakati mwanamke huyo alikuwa mweupe na inaaminika anakaribia miaka 20.

No comments: