DEREVA TEKSI AUA ABIRIA KISHA AENDA KUSTAREHE NA MPENZI WAKE...

JUU: Sian O'Callaghan. CHINI: Christopher Halliwell. KULIA: Polisi wakichukua mwili wa Sian kwenye msitu wa Savernake.
Mpenzi wa zamani wa muuaji Christopher Halliwell amebainisha jinsi walivyoweza kufanya mapenzi masaa machache baada ya dereva teksi huyo kumtesa na kumuua mfanyakazi wa ofisini Sian O'Callaghan.
Heather Widdowson hakuwa akifahamu wakati akiingia kitandani kulala na mpenzi wake huyo mwenye miaka 48 kwamba mwanaume huyo alikuwa amemteka nyara na kumchoma visu Sian mwenye miaka 22 wakati alipokuwa akiendesha teksi yake mjini Swindon mapema asubuhi ya siku hiyo.
"Alinichukua hadi kitandani mchana wa siku hiyo masaa kadhaa baada ya kumuua Sian," alisema mwanamke huyo mwenye miaka 55, wakati akifafanua kuchukizwa kwake baada ya kugundua kitendo kibaya alichofanya Halliwell.
"Sifahamu jinsi gani aliweza kutunza hisia zake mwenyewe lakini nakumbuka alikuwa akicheka na kunitania," alisema.
Mfanyakazi huyo wa ofisini alikuwa akirejea nyumbani kwake anakoishi pamoja na rafiki yake wa kiume baada ya kutoka klabu ya usiku ya Suju iliyoko Swindon ndipo alipopanda teksi ya Halliwell aina ya Toyota Avensis yenye rangi ya kijani.
Badala ya kumpeleka nyumbani, muuaji alimchukua Sian hadi karibu na Msitu wa Savernake ambako alimbaka na kumuua.
Dereva teksi huyo alihukumiwa kifungo cha maisha kwa mauaji yake kwenye Mahakama Kuu ya Bristol, Ijumaa iliyopita.
Heather alieleza jinsi, asubuhi ya baada ya shambulio hilo la mauti, mpenzi wake huyo wa zamani alivyoamka mapema isivyo kawaiwa na kumweleza alikuwa 'na mambo mengi ya kufanya', kabla ya kupeleka teksi yake sehemu ya kuoshea magari.
Sasa ameelewa kwamba kujidamka kwake Halliwell asubuhi ilikuwa ni janja yake ya kujaribu kuficha uhalifu wake huo wa kutisha.
Dereva teksi huyo pia alihamisha mwili wa Sian na kuupeleka huko Uffington, mjini Oxfordshire. Kisha akawapeleka polisi nyumbani kwa Heather baada ya kukamatwa Machi 24, 2011.
Mke wa zamani wa Halliwell, Lisa, ambaye ni nesi, alieleza jinsi muuaji huyo alivyomchukua mtoto wake wa kiume katika teksi yake siku moja baada ya shambulio alilomfanyia Sian.
Alisema mwanaume huyo mwenye miaka 48, ambaye atatumikia miaka isiyopungua 25 gerezani, alipeleka barua ya kuangukia kwa familia yake akiomba wamsamehe.
Heather ambaye alikutana na Halliwell mwaka 2003 na kuendelea naye baada ya mwanaume huyo kuachana na mkewe, alieleza jinsi alivyobandika matangazo ya kupotea kwa Sian kwenye teksi yake aliyotumia kumteka msichana huyo wakati polisi wakimsaka binti huyo wa miaka 22 kufuatia kutoweka kwake.
Akitoa hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 25 jela, Hakimu Laura Cox alisema Halliwell alitumia vibaya nafasi yake kama dereva teksi.

No comments: