CHEKA TARATIBU...

Mwanamke mmoja mlokole alikuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga yenye pande mbili. Upande mmoja alikuwa akiishi yeye na upande mwingine jamaa mmoja. Kila siku yule mwanamke alikuwa akisali kwa sauti na kumalizia, "Asante Mungu!" Kila alipomalizia kusali, jamaa upande wa pili alikuwa akijibu kwa sauti, "Unajisumbua bure, hakuna Mungu!" Siku moja usiku yule Mlokole akasimama nje na kuanza kuomba, "Eeh Mungu, niletee chakula na vinywaji maana leo sina hata senti!" Alipoamka asubuhi akakuta vyakula tele na vinywaji mlangoni kwake. Akapiga kelele, "Asante Mungu!" Yule jamaa akadakia, "Hakuna lolote, vyote hivyo nimekununulia mimi na wala sio Mungu!" Mlokole akainua mikono juu na kusema kwa sauti, "Asante Mungu si kwa chakula tu, bali kwa kumfanya shetani avilipie kabisa!" Duh…

No comments: