CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaenda kwa mganga afundishwe kutabiri. Baada ya kujieleza mganga akamwambia, "Hebu ingiza miguu yako kwenye hicho chungu chenye maji yanayochemka!" Jamaa akajibu kwa mshangao, "Ebo! Unataka niungue?" Mganga akajibu huku akicheka, "Una kichwa chepesi mno, tayari umeshakuwa MTABIRI!" Kasheshe...

No comments: