Kamanda wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas. |
Hali tete ilijitokeza jana katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Daraja Mbili jijini Arusha, baada ya makada wawili wa CCM na Chadema kudaiwa kufyatua risasi hewani.
Makada hao ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nasari na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Wilaya ya Arusha, God Mwalusamba.
Wakati Nasari akikanusha madai hayo na kumtupia mpira Mwalusamba, kada huyo wa CCM alikuwa akiandikisha maelezo yake jana jioni katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha; wakati Nasari na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakisakwa na Polisi kutokana na tukio hilo.
Kata 19 nchini ikiwamo ya Daraja Mbili, jana zilikuwa zikifanya Uchaguzi Mdogo wa madiwani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo za waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo kufariki dunia.
Nasari anadaiwa kuwafyatulia risasi hewani mfululizo na kufanya wananchi waliokuwa wakienda katika kituo cha Shule ya Sekondari ya Felix Mrema kupigia kura, kutawanyika hovyo, hali iliyozua tafrani na vurugu kubwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na wafuasi zaidi ya 10 wa Chadema kukamatwa huku Nasari na Lema wakisakwa baada ya kutoroka kutokana na vurugu hizo.
Waliokamatwa ni Efraim Mmasi, Nicholaus Andrew maarufu ‘Ringo’, Makenzi, mwingine aliyefahamika kwa jina la Snoka na wengine ambao hawakufahamika majina yao mara moja.
Nasari anadaiwa kuanzisha vurugu hizo akiongozana na Lema ambapo kijana wa CCM, Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na mfuasi wa Chadema.
Pia vurugu hizo zilisababisha kushambuliwa kwa kipigo na kuporwa kwa simu ya mkononi na fedha za Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha, Martin Munis na wafuasi hao wa Chadema na tukio hilo limeripotiwa polisi na kupewa namba AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili.
Vurugu hizo zilitokea eneo la Mtaa wa ‘Alinyanya’ jirani na Ofisi ya Mtendaji Kata ya Daraja Mbili baada ya wafuasi wa Chadema kufika katika eneo hilo wakiwa na silaha hizo na kuwazingira wananchi ambao wengi wao walikuwa wafuasi wa CCM walipokuwa wakienda kupiga kura katika kituo hicho.
Kabla ya vurugu hizo, alifika Lema akiwa ndani ya gari aina ya Noah akiwa na Nasari na baadhi ya wafuasi wao ambapo kabla ya gari hilo kusimama, Nasari alishuka na baada ya muda mfupi walifika wafuasi wengine wakiwa katika gari jingine aina ya Toyota Land Cruiser VX mali ya Lema.
Imeelezwa kuwa lengo la kuwazingira wananchi hao ni ili kuwatisha wasipige kura kwa kuhofia vurugu ambapo hata hivyo zimeonekana kuathiri kwa kiasi upigaji kura, huku likishuhudiwa na askari Polisi waliokuwa wamesimama nje la lango la kuingilia shuleni hapo.
Kutokana na kuwapo kwa umati mkubwa wa wananchi, wengi wao wakiwa wafuasi wa CCM, Nasari anadaiwa kutoa bastola yake na kufyatua risasi tatu hewani, jambo ambalo liliwashitua wananchi wakiwamo wafuasi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Alinyanya, Omar Sheikh.
Kutokana na kudhibitiwa, Nasari, Lema pamoja na wafuasi wao walipanda katika magari yao na kisha kuondoka na kuelekea katika ofisi yao ya chama na kuanza kuzungumza na wafuasi wao.
Akizungumzia tukio hilo, Sheikh alisema kutokana na vurugu hizo, wananchi wengi waliingiwa na woga wa kwenda katika vituo vya kupiga kura, hali iliyosababisha kuomba msaada wa kusindikizwa.
Kwa upande wake, Mwalusamba ilibidi apige risasi nne hewani baada ya kudaiwa kuzingirwa kwa silaha za jadi na wafuasi wa Chadema.
Tukio hilo lilizuka saa 5 asubuhi pale wafuasi wa Chadema wakiwa na silaha za jadi, panga, sime, marungu na fimbo, walipowazingira wanachama wa CCM kwa madai kuwa walikuwa na shahada za ziada.
Akizungumzia tukio hilo, mwanachama wa UVCCM, Ramadhani Mkulu ambaye shati lake lote lililowa damu alidai kupigwa risasi hewani na Mwalusamba kuliwaokoa kukatwa mapanga na vijana wa Chadema.
Mkulu alidai mwenzao Kabwele Mturuka amekatwa mkono na panga na wengine kujeruhiwa vibaya.
“Baada ya kuona hali hiyo ikiwa mbaya sana, Mwalusamba alipiga risasi nne hewani, risasi zilizosaidia kwa asilimia kubwa kutuliza jazba, lakini hali ilikuwa tete na kama Mwalusamba asingepiga risasi maafa yangekuwa makubwa zaidi,” alidai Mkulu ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa.
Mwalusamba hakupatikana kueleza tukio hilo kwani alikuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha akitoa maelezo ya kupiga risasi hewani na tukio zima kwa ujumla.
“Si unaniona niko hapa Polisi….subiri kidogo kaka nikitoka hapa ntakutafuta na kukupa taarifa rasmi juu ya hiki ninachoandika hapa,” alisema Mkulu akiwa kituoni hapo.
Kwa upande wake, Nasari alisema yeye hawezi kuwa mpuuzi kiasi cha kupiga hovyo hovyo kwani “sasa nimekua na nina majukumu mengi katika jimbo.”
Alikiri kuwapo katika Kata ya Daraja Mbili, lakini aliyepiga risasi ni Mwalusamba. “Mimi sijapiga risasi kaka, nina akili timamu…siwezi kuwa na akili mbovu kiasi hicho. Mtu aliyepiga risasi ni Mwalusamba,” alidai.
Uchaguzi huo wa Daraja Mbili ulitokana na kifo cha aliyekuwa Diwani wa CCM, Bashir Msangi na ulihusisha vyama vya CCM, Chadema, NCCR- Mageuzi, TLP na CUF. Wakati tukienda mitamboni, matokeo ya awali yalionesha kuwa CCM ilikuwa imeachwa nyuma na Chadema katika vituo vyote 39.

No comments:
Post a Comment