Mmoja wa tembo katika Hifadhi ya Serengeti. |
Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti, wilayani hapa, akiwamo aliyenyweshwa dawa ya kienyeji, baada ya kukiri kosa la wizi wa miwa ya mwanakijiji mwenzake, na mwingine kwa kuuawa na tembo wakati akifanya uwindaji haramu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Vyombo vya usalama wilayani hapa vimesema tukio la kwanza lilitokea Oktoba 24 saa 3 asubuhi katika kijiji cha Salama Kati, ambapo wachungaji wawili wa ng’ombe, Edwin Revocatus (19) na Mugisha Jackson (17) walituhumiwa kuiba miwa katika shamba la mwanakijiji mwenzao.
Ilielezwa kuwa mwenye shamba hilo, Warioba Makanga aliwakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya kijiji hicho ambako walikiri kosa na kuomba msamaha.
Ilidaiwa kuwa baada ya kutoka ofisini hapo, mwenye shamba hilo alitafuta mganga wa kienyeji kijiji jirani na mganga huyo kuja kuwanywesha dawa watuhumiwa hao, kama ishara ya kuapa kutorudia kosa na kuachana kabisa na wizi.
“Mganga huyo aliwanywesha dawa hiyo na baada ya kuinywa hali zao zilibadilika,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Aidha, ilielezwa kuwa baada ya kunywa dawa hiyo matumbo ya wafugaji hao yalijaa, na muda mfupi baadaye Revocatus alipoteza maisha huku Jackson akikimbizwa katika Kituo cha Afya Nyamuswa, ambako bado amelazwa.
Vyombo vya ulinzi na usalama wilayani hapa vilisema kutokana na hali hiyo, wananchi wa kijiji hicho walijichukulia sheria mkononi kwa kubomoa nyumba za mmiliki wa shamba hilo.
Aidha, ilielezwa kuwa watuhumiwa hao ambao ni Warioba Makanga na Makanga Makanga, baada ya tukio hilo walitoroka na wanatafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika tukio lingine la usiku wa Oktoba 24, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Maduhu Baraka (55), mkazi wa kijiji cha Nyamatoke, wilayani hapa, aliuawa na tembo kwa kuchomwa na pembe tumboni wakati akifanya uwindaji haramu katika hifadhi hiyo.
Ilielezwa kuwa mwananchi huyo alikuwa akiwinda na wenzake ambao hawajajulikana na kwamba wenzake walikimbia baada ya mnyama huyo kumshambulia mwenzao.
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wilayani Bunda ambaye hakutaka kutajwa kutokana na kwamba yeye si msemaji wa Jeshi hilo, alithibitisha kusikia matukio hayo lakini akasema hawezi kulitolea ufafanuzi.

No comments:
Post a Comment