AJALI YAUA WATU WATANO NA KUJERUHI 14 DODOMA...

Kamanda Zelothe Stephen.
Watu watano wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka jana jioni katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Bahi Relini ambapo gari lenye namba za usajili T803 ABX Toyota Hiace iliyokuwa ikiendeshwa na Yohana Samson ikitokea Dodoma kwenda Makanda, iliacha njia na kupinduka.
Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa ni gari lenye namba za usajili T518 AVQ Scania iliyokuwa  ikiendeshwa na Tutu Jackson ilitaka kuipita Toyota Hiace na kisha kurudi barabarani ghafla na kisha kugonga ‘Kipanya’ hicho ambacho kilipinduka.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bahi, Ramadhani Kitanto aliyekuwa eneo la tukio, alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo na majeruhi, lakini hata hivyo hakutaka kusema chochote kwani msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen.
“Ni kweli ajali imetokea mimi si msemaji, wasiliana na Kamanda,” alisema Kitanto.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Zelothe Stephen aliahidi kutoa taarifa rasmi leo. “Ni kweli ajali imetokea, lakini nitatoa taarifa kesho,” alisema.
Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa  Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya alisema kuwa bado hawajapokea majeruhi wala maiti. “Kama ajali imetokea jioni hii nadhani wanafanya utaratibu wa kufikisha majeruhi na maiti hospitalini hapa,” alisema.

1 comment:

Anonymous said...

I just couldn't depart your web site before suggesting that I really enjoyed the standard information a person provide for your visitors? Is gonna be back often to check up on new posts