ABAMIZA GARI LAKE LA PAUNI 75,000 KWENYE BASI NA KUFA PAPO HAPO...

Hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.
Mtu mmoja amekufa baada ya gari lake la michezo lenye thamani ya Pauni za Uingereza 75,000 alilokuwa akiendesha kujibamiza kwenye basi.
Kifusi kilisambaa barabarani baada ya gari aina ya Audi R8 nyeupe kugongana uso kwa uso na basi la Arriva mjini Newcastle juzi usiku.
Dereva huyo mwenye miaka 39 alilazimika kutolewa kwa kukatwa sehemu ya gari lake na wafanyakazi wa dharura, lakini alithibitika kufa katika eneo la tukio. Dereva wa basi hilo mwenye miaka 61, alikimbizwa hospitali kufuatia kupata majeraha madogo.
Hakukuwa na abiria kwenye basi hilo wakati ilipotokea ajali hiyo karibu na Mtaa wa Gosforth High.
Wageni waliopanga katika hoteli ya jirani ya Gosforth waliokuwa wakirejea kutoka kwenye baa walishuhudia ajali hiyo mbaya, alisema Mfanyakazi wa Hoteli ya Gosforth.
"Tulikuwa na wateja kadhaa ndani ambao walikuwa wanakunywa kwenye baa nyingine na kushuhudia ajali hiyo. Walisema dereva alitolewa baada ya kukatwa sehemu ya gari lake lakini madaktari hawakuwa na la kufanya zaidi kuokoa maisha yake," alisema mfanyakazi wa kike.
Tony Batty, Mkuu wa Huduma wa Arriva alisema: "Tunazo taarifa za tukio hilo kati ya gari dogo na basi la Arriva huko Mtaa wa Gosforth High.
"Dereva wa gari dogo alifariki. Tunazipa pole familia za dereva wa basi na dereva wa gari dogo. Tukio limehusisha basi ambalo halikuwa kwenye huduma na dereva amepelekwa hospitali kwa matibabu."
Polisi wa Northumbria walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya Saa 3:00 usiku wa Jumapili pale magari mawili yaliyokuwa yakisafiri kutumia njia moja, ambapo yalisababisha barabara hiyo kufungwa kwa  kwa masaa matano.

No comments: