MWANAMKE AMCHINJA MTU ALIYEMBAKA NA KUMPA UJAUZITO...

KUSHOTO: Uwanja ambako kichwa cha mbakaji kilitupwa. JUU: Nevin Yildirim. CHINI: Nurettin Gider.
Huyu ni mwathirika wa tukio la kubakwa mjamzito ambaye alimpiga risasi na kumkata kichwa mbakaji kisha kukitelekeza kichwa kwenye uwanja wa kijijini kwake.
Nevin Yildirim mwenye miaka 26, sasa anasubiri hukumu baada ya kumuua mwanaume nyumbani kwake Yalvac, kusini-magharibi mwa uturuki wiki iliyopita.
Mama huyo wa watoto wawili ni mjamzito wa miezi mitano, ambayo amedai ni ujauzito wa mbakaji huyo.
Anataka mamlaka husika kumruhusu aitoe mimba hiyo licha ya kwamba ameshapita kwa wiki nne muda wa wiki kumi unaoruhusiwa nchini Uturuki kufanya hivyo.
Yildirim alisema mwanaume huyo, Nurettin Gider, alianza kumshambulia siku chache baada ya mumewe kuondoka nyumbani Januari kwenda kufanya kazi za msimu katika mji mwingine.
Alidai mwanaume huyo alimtishia kwa bunduki na kusema angewaua watoto wake, wenye umri wa miaka miwili na sita, kama asingekaa kimya, imeripotiwa.
Ubakaji uliendelea tena kwa miezi minane iliyofuatia hadi Agosti 28, pale Yildirim alipoamua kwamba liwalo na liwe, kwa maana sasa imetosha.
Siku hiyo alimpiga risasi Gider baada ya kuparamia ukuta wa nyuma ya nyumba yake na kisha tena akampiga risasi alipojaribu kuchukua bunduki yake.
Alisema: "Nilimkimbiza, alianguka chini. Alianza kuniapiza.
"Nilimpiga risasi sehemu zake za siri safari hii. Akanyamaza kimyaa. Nilijua alikuwa amekufa. Kisha nikakata kabisa kichwa chake."
Kwa ujumla, Yildirim alimpiga risasi mara kumi, ikiwamo mara kadhaa kwenye eneo viungo vyake vya uzazi. Pia aliripotiwa kuchomwa visu kwenye utumbo wake mkubwa baada ya kuwa amepigwa risasi.
Kisha akachukua kichwa chake, ambacho kilikuwa kikichuruzika damu, kwenye nywele hadi katika uwanja wa kijijini huko Yalvac, walioshuhudiwa walisema.
Akiongea na wanaume waliokuwa wameketi nje ya mgahawa, alisema: "Msinitete, msicheze na heshima yangu. Hiki ni kichwa na mwanaume ambaye alichezea heshima yangu."
Picha za video za kichwa na Gider kikiwa chini zilipigwa na mtangazaji wa kituo binafsi cha DHA, ambaye aliwasili eneo la tukio kabla ya polisi.
Inadhaniwa kuwa mbakaji alimsaliti Yildirim. Alisema alimpiga picha cha utupu wakati wakiwa mjamzito baada ya kupenyeza kimya kimya kwenye chumba chake usiku. alimtishia kuzisambaza kwa wazazi wake isipokuwa tu akiendelea kulala naye, alisema.
"Aliendelea kusema kwamba angemweleza kila mtu kuhusu ubakaji huo, "Yildirim aliripotiwa akisema wakati wa kutoa ushahidi.
"Binti yangu ataanza shule mwaka huu. Kila mmoja angeweza kuwatusi watoto wangu. Sasa hakuna atakayeweza kufanya hivyo.
"Nimeokoa heshima yangu. Sasa watawaita wanangu watoto wa mwanamke aliyepigania heshima yake."
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuliwa, Yildirim alisema: "Nilifikiria kumripoti kwa jeshi la polisi na kwa mwanasheria wa wilaya, lakini hii ingenifanya nionekane kama mwanamke aliyedharauliwa.
"Kutokana na kuelekea kupata sifa mbaya nikaamua kusafisha heshima yangu na kuamua kumuua. Nilifikiria sana kujiua lakini sikuweza kufanya hivyo."
Kikundi cha wanawake nchini Uturuki wamemfagilia Yildirim kama heroine.
Yildirim amefikia kusema kwamba anajiandaa kufa kwakuwa anaruhusiwa kutoa mimba.
Baba wa watoto wawili, Gider ambaye ana miaka 35, alifunga ndoa na shangazi wa mume wa Yildirim.

No comments: