MWANAMKE ALIYEMTONGOZA MWANAFUNZI KUFUNGWA MIAKA 14...

Mwanamke ambaye alikiri kumtongoza mvulana wa chini ya miaka ishirini amelazimishwa kujiorodhesha kama mhalifu wa ngono na kwamba anakabiliwa na kifungo cha miaka 14 gerezani.
Marie Friendship mwenye miaka 38, alipatikana na hatia katika shitaka moja la kujihusisha na vitendo vya ngono na mtoto, kati ya jumla ya mashitaka manane.
Hatia ya Marie iliyopatikana kwenye shitaka moja imekubaliwa na Waendesha Mashitaka (CPS) wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Bristol.
Alielezwa kujiorodhesha kama mhalifu wa ngono, wakati Jaji akiahirisha hukumu kwa ajili ya kupisha muda wa kuandaa ripoti.
Richard Posner, mwendesha mashitaka wa CPS, alisema Mahakama itafikiria kutumia Amri ya Kinga ya Makosa ya Ngono (SOPO).
Amri kama hiyo inaweza kutumika kuepusha mtuhumiwa kukaribiana na vijana wadogo.
Robert Duval, akitetea alisema: "Haya ni mashitaka mazito na nakubaliana na kesi hii. Tungependa kupata ripoti ya mwanzo ya hukumu. Huyu ni msichana ambaye alikuwa na rekodi nzuri hapo kabla."
Marie ambaye anaishi Whitchurch, mjini Bristol, aliwekewa dhamana, kusubiria ripoti, kwa ajili ya hukumu itakayotolewa Septemba 21, mwaka huu.
Aliwekewa dhamana kwa sharti kwamba asimkaribie kabisa mlalamikaji.
Mtunza kumbukumbu wa Jaji wa Bristol, Neil Ford alimweleza mwanamke huyo: "Ukweli ni kwamba ninapoahirisha kesi kungojea ripoti si dalili kwamba hukumu imeondolewa dhidi yako kutokana na tukio hili.
"Ukweli ni kwamba kupatiwa dhamana si dalili za kuhukumiwa."
Marie, ambaye aliwawekea alama Harry Potter na David Beckham ya 'kukubali' kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, aliorodheshwa kuwa kwenye mahusiano katika tovuti ya mtandao wa kijamii.

No comments: