MKE WA BOBBY BROWN AUGUA KIFAFA HOTELINI...

KUSHOTO: Bobby akiwa na mkewe, Alicia. KULIA: Bobby na mkewe Alicia siku ya harusi yao.
Mke wa Bobby Brown amelazwa hospitali baada ya kuugua kifafa usiku wa Jumamosi, kwa mujibu wa ripoti.
Nyota huyo wa kundi la New Edition alikuwa akirekebisha vifaa vya muziki kwa ajili ya onesho la kundi hilo mjini Florida lililotarajiwa kufayika jana usiku ndipo Alicia Etheredge alipopatwa na kifafa akiwa katika chumba cha hoteli walimofikia, imeripotiwa.
Wawili hao wamefunga ndoa miezi mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa tovuti ya nyota huyo, Alicia alichukuliwa kwenye gari la wagonjwa hadi hospitali moja, ambako alikutana na Bobby.
Kundi la New Edition lilipanga kufanya onesho Saa 3 usiku katika tamasha la 10th Annual Tom Joyner Family Reunion kwenye ukumbi wa Gaylord Palms Resort mjini Orlando, kuadhimisha miaka 30 ya kundi hilo.
Iliripotiwa mapema mwezi uliopita kwamba, mume huyo wa zamani wa Whitney Houston alikuwa akipatiwa matibabu kuachana na ulevi wa kupindukia lakini akakatisha kabla ya kumaliza programu hiyo.
Mwimbaji huyo mwenye miaka 43 anaaminika alitumia wiki zisizozidi tatu kwenye taasisi moja ambayo haikuweza kufahamika ambako alikubali kupata tiba hiyo kufuatia kukamatwa kwake kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa Machi, mwaka huu.
Bobby na Alicia, ambaye pia ni meneja wake, walivishana pete mwaka 2010, miaka mitatu baada ya Bobby kutalikiana na Whitney, mwimbaji wa 'I Will Always Love You'.
Wawili hao walifunga ndoa mbele ya familia na marafiki wa karibu chini ya masaa 24 baada ya kutumbuiza kwenye tamasha la New Edition mjini Honolulu, Juni, miezi minne baada ya kifo cha Whitney.
Mtoto wa kiume wa wanandoa hao, Cassius mwenye miaka mitatu alisimamia ndoa hiyo. Watoto wakubwa wa Bobby, Landon mwenye miaka 23, La'Princia mwenye miaka 22 na Bobby Jr. mwenye miaka 19, wote pia walihudhuria lakini binti yake, Bobbi aliyezaa na Whitney, hakutokea kwenye harusi hiyo.

No comments: