HUU NDIO UNYAMA WA WAPIGANAJI WA TALIBAN...

KUSHOTO: Wapiganaji wa Taliban wakiwa mesimama mbele ya vichwa vya askari waasi. KULIA: Mullah Dadullah.
Picha hii ya kuhuzunisha inaonesha wapiganaji wa Taliban wakiwa wamesimama mbele ya vichwa vilivyokatwa ambavyo vinadaiwa kuwa ni vya askari waliouawa katika mapigano kwenye mpaka wa Pakistani.
Taliban wa Pakistani wamesambaza video inayoonesha kile kinachoonekana kuwa ni vichwa vya askari kadhaa jana huku maofisa usalama wakisema wanajeshi 15 hawajulikani walipo kufuatia mapigano makali dhidi ya askari waasi.
Mapigano ya jumanne yamekuja kama sehemu ya oparesheni ya majeshi ya Pakistani kufukuza wapiganaji wa Taliban ambao wamevuka mpaka kutoka Jimbo la Kunar nchini Afghanistan Ijumaa iliyopita na kutwaa kijiji cha Batwar kilichopo wilaya inayokaliwa na watu wa kabila la Bajaur.
"Takribani askari wetu 15 wamepotea," ofisa wa juu wa usalama alilieleza Shirika la Habari la AFP.
Ofisa Usalama mwingine alisema ‘pungufu au zaidi’ kwamba askari wengi walikuwa hawajulikani walipo lakini akakataa kutaja idadi kamili.
Msemaji wa Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), Sirajud Din alituma video kwa AFP inayoonesha kamanda wa vikosi akiwa kasimama mbele ya vichwa 12 vilivyopangwa ardhini ambavyo inadaiwa vilitokana na ashari waliokuwa wamewaua.
"Mungu ashukuriwe kwamba mujahidina huko Bajaur wameweza kuwaua askari kafiri wa Pakistani," alisema.
"Wengi wao waliuawa kwa risasi, 12 kati yao kama unavyoona wamekatwa vichwa, unaona vichwa 12 hapa, na vichwa zaidi vinakuja." Kamanda, sura yake ikiwa imefichwa na kuvalia vazi la kiasili, anaonekana kwenye video hiyo akiwa kazingirwa na wapiganaji kadhaa wenye silaha akiwamo mmoja aliyeshikilia shoka kubwa sana.
Viseo hiyo inaonesha mali za askari waliokatwa vichwa zikiwa zimewekwa kwenye shuka, ikiwami vitambulisho vya Pakistani, kofia za chuma, fedha za Pakistani, simu za mikononi na kadi za benki.
Vyanzo vya habari kutoka jeshini kwa sasa havikusema kama kuna askari waliopotea au kuthibitisha kwamba wote waliooneshwa kwenye video ni askari wa Pakistani.
Msemaji alisema wamekuwa wakiuawa kulipiza 'ukatili' unaofanywa na askari wa Pakistani.
Julai, TTP ilitoa video inayoonesha vichwa 17 vya askari wa Pakistani waliodai kuuawa kwenye mapambano mpakani huko katika wilaya ya kaskazini-magharibi ya Upper Dir.
Maofisa wa Usalama wa Taifa wameshutumu shambulio hilo dhidi ya Wapakistani watiifu kwa Maulana Fazlullah, ambao walikimbilia Afghanistan baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi katika udhibiti wa bonde la Swat.
Mapigano huko Bajaur katika wiki iliyopita yamesababisha vifo vya watu takribani 50, wakiwamo wapiganaji 31 na wafuasi wawili wa tume ya serikali ya kurejesha amani ambao waliuawa Jumatatu.
Wiki iliyopita, mashambulizi ya ndege za majeshi ya NATO huko mashariki mwa Afghanistan yalimuua Kiongozi wa Taliban nchini Pakistani ambaye alikuwa akishirikiana kwa ukaribu na al-Qaeda.
Mullah Dadullah aliuawa Ijumaa katika Jimbo la Kunar nchini Afghanistan, ambalo lipo mpakani kutoka eneo linalokaliwa na watu wa kabila la Bajur, msemaji wa majeshi ya mseto alisema.
Alikuwa ni kiongozi wa Taliban Pakistani mjini Bajur, na NATO walisema Jumamosi kwamba Dadullah alikuwa akiongoza mapambano ya askari na silaha mstari wa mbele pamoja na mashambulizi dhidi ya vikosi vya Afghanistan.
Bajaur ni moja kati ya wilaya saba katika ukanda wa kikabila nchini Pakistani, ambako wapiganaji wanaojihusisha na Taliban na al-Qaeda wamejikita na kupatumia kuandaa mashambulizi huko Pakistani.
Pakistani imepoteza zaidi ya askari 3,000 katika mapambano dhidi ya askari waasi nchini humo lakini imekataa shinikizo kutoka Marekani kutumia nguvu kuondosha makimbilio yanayotumiwa na wote wanaopambana dhidi ya Wamarekani nchini Afghanistan.

No comments: