JUU: Picha iliyopigwa kutoka ghrofani ulipo mgahawa wa Coq D'Argent.CHINI: Sehemu ambapo mwanamke huyo aliangukia kwenye Kituo cha basi cha Bank. KULIA: Mmiliki wa mgahawa huo, Sir Terence Conran.
Mfanyabiashara wa kike ameporomoka na kufa urefu wa futi 80 kutoka kwenye paa la mgahawa uliopo eneo la wazi juu ya jengo lenye ofisi mbalimbali mjini London juzi. Msichana mwenye asili ya Asia aliyevalia kinadhifu alianguka ghorofa nane kutoka juu ya mgahawa unaomilikiwa na Sir Terence Conran wa Coq D'Argent majira ya Saa 12:30 jioni, na kutua mbele ya mamia ya abiria nje ya Kituo cha Bank.
Shuhuda wa tukio hilo alisema alikunywa mvinyo kwenye glasi yake katika eneo la juu katika Jiji, kabla ya kutua mkoba wake sakafuni na kisha kukwea mpaka juu kabisa ya mgahawa.
Wapitanjia na wahudumu wa afya walijaribu kuokoa maisha yake, lakini alithibitika kufariki dunia. Mwathirika huyo alielezewa kama aliyevalia nadhifu japo alikuwa amevalia sweta, suruali na raba.
Polisi waliwasili na wateja wakalazimika kuondoka kwenye mgahawa huo wa Coq d'Argent.
Mteja mmoja katika mgahawa huo, ambaye alionekana kwenye mwandamano wa James Bond kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Olimpiki ambazo zilimhusisha Malkia, alieleza kwamba watu walikuwa wakizungumza na kula ndipo mwanamke huyo alipokwea juu.
Alisema: "Ghafla mgahawa ukawa kimya na wafanyakazi wakasema tunatakiwa kuondoka. Ilikuwa inatisha sana."
Mgahawa huo ulionekana kwenye filamu kama Her Majesty, ubavuni mwa mwigizaji wa James Bond, Daniel Craig, inavyoonekana aliruka kuelekea Uwanja wa Olimpiki mjini Stratford, ambako aliruka kwa 'mwavuli' kuingia katika sherehe za ufunguzi. Wateja waliokuwa wakila walionekana wakipungia mikono helikopta.
Ni kifo cha tatu kutokea kwenye mgahawa huo, ambao uko juu ya jengo linalotumiwa na kampuni ya Aviva Investments.
Mei 2007, mwajiriwa wa Jiji, Richard Form mwenye miaka 33, alikufa baada ya kujibamiza kutoka mahali palipoinuka na kutua juu ya basi.
Julai 2009, Anjool Malde mwenye miaka 24 aliruka na kufa kutoka eneo hilo akiwa kashikilia glasi ya shampeni baada ya kuwa kasimamishwa kazi katika Benki ya Deutsche.
Mmoja wa walioona tukio hilo alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema: "Moyo wangu haukuwahi kudunda hivi na kwa kasi katika maisha yangu yote. Watu walikuwa wakilia huku macho yao yakitazama nje. Alitua umbali wa mita 20 mbele yangu.
"Bado siamini jinsi nilivyokuwa jirani na tukio zima, sidhani maisha katika Jiji hili yapo kwa ajili yangu. Namaanisha jinsi gani mambo yalivyokuwa mabaya kwake?"
Msemaji wa Polisi wa Jiji la London alisema: "Katika muda unaokadiriwa kuwa Saa 12:30 jioni mwanamke alionekana akianguka kutoka kwenye jengo huko Poultry. Alithibitishwa kufariki eneo la tukio."
David Loewie, Mkurugenzi Mtendaji wa D&D London, ambayo inamiliki Coq d'Argent, alisema: "Ni tukio la kuhuzunisha mno, lakini hatuwezi kusema chochote zaidi wakati uchunguzi wa Polisi unaendelea."
Coq d'Argent inahudumia vyakula vya hali ya juu wa Kifaransa kwenye mgahawa wake uliopo sehemu ya juu ya jengo ambayo ina bustani ambapo unaweza kuona sehemu kubwa ya Jiji.
No comments:
Post a Comment