KUSHOTO: Shaurya. KULIA: Hospitali ambako Shaurya amekuwa akipatiwa matibabu baada ya mateso makali kwa miaka takribani 10.
Wazazi wa mvulana mmoja ambao walishiriki kumfanyia kila aina ya mateso, sasa wanakabiliwa na adhabu ya kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuua.Udhalilishaji ulianza pale Shaurya alipokuwa na miaka mitatu na kumpatia haki yake, sasa ana miaka 13, alikuwa akipigania kuishi kwa babu na bibi yake.
Mama yake alifariki wakati akiwa mdogo hivyo akalazimika kuishi na baba yake, Lalit Balhara ambaye ni Meja wa zamani wa jeshi, na mama yake wa kambo, Preeti Balhara.
Wakati wa kesi, Shaurya inasemekana aliteswa mara kwa mara na wawili hao na alidaiwa mara kadhaa kufungiwa chumbani bila chakula na kuchapwa kwa fimbo kama angejaribu kulia, imeripotiwa.
Pia imedaiwa kuwa walipachika fimbo mdomoni mwake ambayo ilisababisha kuvunjika baadhi ya meno yake.
Wawili hao walikana madai hayo, wakisema mtoto huyo alikuwa wa 'kipekee' tangu kuzaliwa kwake.
Walidai alipata majeraha hayo baada ya kuanguka kutoka kwenye kiti na meza, lakini ripoti ya madaktari iliyoambatanishwa na maelezo ya mtoto huyo imethibitisha kwamba wana hatia.
Shaurya aliendelea kupata mateso, wakati akiwa na miaka mitatu alikimbizwa hospitali kwa kunywa dawa ya kuua wadudu.
Baada ya tulio hilo, matesho yaliendelea na alipata majeraha ya kuvunjika mbavu, kuvuja damu kwenye fuvu na kung'olewa meno, huku uzito wake ukiendelea kupungua siku hadi siku.
Juzi wawili hao walishitakiwa kwa jaribio la kuua na pia walitiwa hatiano chini ya Sheria ya Haki ya Watoto.
Hukumu hiyo ilikuwa tukio la ushindi kwa babu na bibi wa Shaurya ambao walitafuta ulinzi wa mtoto huyo mwaka 2005 wakimtuhumu baba yake, Lalit Balhara na mkewe, Preeti, walikuwa wakimtesa mtoto baada ya mama yake kufariki.
Wakati Shaurya alipopelekwa mbele ya mahakama Februari 20, 2005, muonekano wake wa kimwili na kiakili uliwashitua maofisa, kwa mujibu wa magazeti.
Madaktari walitakiwa kutoa ripoti ya matibabu na Meja Balhara na mkewe walipelekwa kupimwa akili katika Hospitali ya Jeshi, Delhi Cantontment.
Ripoti ilieleza 'wazazi hao walishindwa kueleza kwa nini mtoto alikuwa na majeraha na kuhitimisha kwamba Shaurya alikuwa akisumbuliwa na 'dalili za maradhi ya watoto' - mchanganyiko wa majeraha mwilini kama kuvunjika mifupa, majeraha ya moto na utapiamlo vilivyosababishwa na mateso kutoka kwa wazazi au mwangalizi.
Februari 2005, Shaurya alipatiwa ulinzi kwa babu na bibi yake.
Adhabu kwa jaribio la kuua ni kifungo cha maisha jela na wawili hao watajua hatima yao wiki hii. Mapema baada ya hukumu kutangazwa, akina Balhara ambao walikuwa nje kwa dhamana wakati wote wa mashitaka, walipelekwa rumande.
No comments:
Post a Comment