WAKATI MAMA AKITANGAZA KUFILISIKA, BINTI ANYAKUA DHAHABU OLIMPIKI...

Miezi michache tu kabla ya Gabby Douglas kushinda medali yake ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini London na kufungua nafasi lukuki ambazo bila shaka zinamwezesha kuvuna mamilioni ya dola, mama yake alitangaza rasmi kufilisika, imefahamika.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana mapema mwaka huu mjini Virginia, zinaeleza kuwa Natalie Hawkins ana mali zisizohamishika zenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani 163,706.10 na kwamba anadai madeni yenye thamani ya Dola za Marekani 79,754.14.
Wanaomdai ni pamoja na:
Capital One....................Dola za Marekani 1,534
Student Loan.................Dola za Marekani 4,350.23
Sprint.............................Dola za Marekani 158.78
T-Mobile........................Dola za Marekani 413
Orthodontist ya Iowa (ambako Gabby alikuwa akijifua wakati akiwa na miaka 14) Dola za Marekani 408.
Hawkins amekubali kufanya utaratibu wa kila mwezi kulipa fedha hizo. Alianza kulipa malipo ya Dola za Marekani 408 kila mwezi tangu Februari mwaka huu...kwa mdhamini ambaye atagawanya fedha hizo miongoni mwa wadai wake.
Hatahivyo, kufuatia umaarufu wa Gabby kwa sasa na uwezekano wa kuvuna mamilioni kupitia mikataba mbalimbali na zawadi, ni wazi mama yake hana sababu ya kuhofia kuhusu kufilisika au kwa lugha nyepesi matatizo ya pesa sasa itabaki kuwa ndoto.

No comments: