Mwanamuziki mashuhuri wa siku nyingi ambaye ni kipofu, Stevie Wonder amewasilisha mahakamani madai ya kutaka talaka, imeelezwa.
Katika nyaraka za talaka zilizopatikana, mwanamuziki huyo ameelezea tofauti ambazo haziwezi kusuluhishwa ndio sababu ya kuchukua uamuzi huo. Kwa mujibu wa nyaraka, Wonder amekuwa mbali na mkewe Kai Millard Morris tangu Oktoba mwaka 2009.
Wonder amewasilisha madai ya talaka akitumia jina lake la kisheria la Stevland Morris, na kusainiwa kwa alama za vidole gumba viwili.
Katika nyaraka, zilizowasilishwa na malkia wa disso, Laura Wasser, Wonder anataka uwepo uangalizi wa pamoja wa watoto wao wawili wa kiume, wenye miaka 10 na 7.
Kwa mujibu wa nyaraka, Wonder ameafiki kulipia gharama zote za mke na malezi ya watoto.
Ingawa Wonder amechuma mali yake kitambo kabla ya kufunga ndoa na Kai mwaka 2001, baadhi ya mali zitagawanywa ...japo nyaraka zimeonesha kiasi bado hakijawekwa bayana kwa sasa.

No comments:
Post a Comment