SALA ZAMWOKOA BIBI WA MIAKA 73 KUBAKWA NA MAJAMBAZI

Bibi kizee mmoja sasa anahofia maisha yake baada ya majambazi kuvunja uzio na kuingia kwenye nyumba yake yenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 7 na kumtia kwenye mateso ya kwenye maji.
Francoise Jansen mwenye miaka 73 alikalishwa mbele ya maji yanayochemka baada ya kuvuliwa nguo zake zote na wanaume ambao walitishia kumkata vidole vyake kama hatofungua sanduku lake la kuhifadhia pesa.
Wanaume wawili walioficha sura zao walitumia ngazi kuingia kwenye nyumba ya mjane huyo kupitia dirisha la chumbani. Walishuka ngazi za nyumba hiyo na kumshangaza bibi huyo ambaye alikuwa akifuatilia michezo ya Olimpiki kwenye televisheni.
Baada ya kupora vito vyenye thamani ya zaidi ya Pauni za Uingereza 150,000 kwenye sanduku wakamtaka afungue sanduku la pili kubwa zaidi lililokuwa chini ya ngazi.
Lakini sanduku, ambalo lilikuwa tupu, halikuwahi kutumika kwa miaka 12 na Francoise hakuweza kufungua licha ya kukumbuka namba za siri.
Hatua hiyo ilipelekea masaa matatu ya mateso makali ambapo wavamizi hao walitumia maji yanayochemka, aina ya mateso ambayo mlengwa anafanywa kujihisi kwamba wanakaribia kumzamisha.
Wanaume hao walichukua nguo ya ndani kutoka chumbani kwa Francoise na kuisokomeza kwa nguvu mdomoni kwa bibi huyo kabla ya kumburuta hadi bafuni. Walimvuta kichwa chake kwa nyuma hadi katika bafu na kumfunika uso wake kwa taulo wakaliloweka kwenye maji yaliyokuwa yakimiminika kutoka kwenye bomba.
"Walinifanyia hivyo mara tatu lakini sikuweza kufungua sanduku," alisema bibi huyo. "Niliendelea kuwaeleza lilikuwa tupu lakini hakuniamini kabisa."
Francoise, ambaye anaishi kwenye shamba lake huko Weybridge, mjini Surrey, alieleza: "Nimeogopeshwa mno, nilihisi wanakaribia kuniua.
"Waliniuliza ama ninfa mjukuu yeyote, nikawaambia ninao kumi na wakasema "Tunakuua, unadhani wajukuu zako watakulilia?"
"Nilificha hofu yangu. Ilikuwa mbaya sana na nilichoweza kukumbuka ni kusali."
Nyumba yake yenye vyumba sita vya kulala ilishawahi kuvamiwa wiki kadhaa zilizopita kabla ya shambulio hilo la Ijumaa na Polisi wa Surrey wanaamini wahusika waliyaona masanduku hayo nyumbani hapo.
Francoise, ambaye alitumia sehemu ya muda wake kabla ya mateso hayo kukaa na marafiki zake kwenye uzio wa viwanja vya Olimpili, alisema wanaume hao kwanza walimshambulia chumbani.
"Mmoja tao aliniinamisha kichwa chini kwa nguvu kitandani huku wengine wakishuka chini liliko sanduku," alisema.
"Aliendelea kusema una pesa zozote na nikaendelea kumweleza sina.
"Huku nikijaribu kubonyesha kitufe cha kengele ya dharura, nilikuwa mbali nacho lakini waliweza kuona nini nilichokuwa nikijaribu kufanya na tangu hapo wakaanza kuwa na hasira kikwelikweli."
Wavamizi hao walichukua sufuria jikoni na kuchemsha maji mgongoni mwake na mkononi lakini Francoise aliendelea kushindwa kuwasaidia kufungua sanduku.
Baada ya mateso hayo ya maji, mmoja wa wavamizi hao akatishia kumkata moja ya vidole vyake lakini mwingine akapiga kelele: "Hapana, atatokwa na damu nyingi hadi kufa."
Francoise alisema: "Kisha wakanifunga na ufito wa taulo pamoja na waya wa redio iliyokuwa jirani, wakakata suruali yangu na fulana kwa kutumia mikasi.
"Nilikuwa nikitetemeka maana nilihisi wanataka kunibaka na nikabaki nikiendelea kusali.
"Nilikuwa nusu mahututi lakini hatimaye nikagundua kuwa wameshaondoka na nikalazimika kujifungua kamba na nyaya zile kwa meno.
"Siwezi kuelezea nafuu niliyopata baada ya polisi kuwasili."
Francoise amekuwa akiishi peke yake kwenye hekalu hilo tangu mumewe Peter, mfanyabiashara, kufariki ghafla mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 58.
Lakini sasa amekuwa mwoga mno kurejea kwenye nyumba yake na amepanga kuishi na mtoto wake wa mwisho, Chris.
Kijana huyo mwenye miaka 42, ambaye ni Ofisa wa Juu wa kampuni ya British Gas alisema: "Tunaimani kubwa kwamba wahusika wa tukio hili wanakamatwa hivyo kuhitimisha suala hili la mama.
"Na pia sababu watu hawa watashambulia tena na hivyo kuwa hatari zaidi. Mama yangu ana bahati sana kubaki hai, mtu sulani alilazimika kufanya aendelelee kuishi."

No comments: