Wakati mtoto wake wa kiume mwenye mwaka mmoja alipoopolewa akiwa nyang'anyang'a tayari akiwa amekufa kwenye bafu lililojaa maji, mlevi Danielle Reeves alipiga kelele kwa ukali na kuwashutumu wote waliomzingira.
Aliwadanganya madaktari wa huduma ya kwanza na pia kusema mtoto wake mwingine mwenye miaka mitatu alikuwa akihusika katika tukio hilo.
Lakini pamoja na yote hayo, akihukumiwa kifungo cha miaka takribani minne juzi, mama huyo kijana mwenye watoto wawili anatakiwa kukabiliana na ukweli kwamba mtu pekee wa kulaumiwa kwa hakika: yeye mwenyewe.
Danielle alimwacha mtoto wake mdogo Frankie Joe kwenye bafu, wakiwa peke yao na kaka yake Alfie kwa ajili ya kumchunga, wakati yeye akitumia dakika 45 kupiga soga na majirani zake nje ya nyumba yake huko Redhill mjini Surrey. Alimweleza mtu mmoja kuwa alikuwa amelewa mno kutokana na kunywa vodka.
Wakati mama huyo mwenye 'mdomo mchafu', mvuta mihadarati ambaye ana miaka 24 alipojisikia kwenda kuwaona watoto wake ndani, maji yalikuwa yamejaa bafuni na kufurika nje.
Frankie alifia hospitalini siku nne baadaye, ikiwa ni siku moja baada ya sherehe yake ya kwanza ya kuzaliwa kwake.
Juzi Danielle, ambaye alikiri kuua bila kukusudia alipofikishwa mahakamani mwezi uliopita, alikuwa akilia kwa kwikwi wakati akisomewa hukumu.
"Umetelekeza kabisa majukumu yako kama mama wa mtoto wakati wa kuoga," alisema Jaji Christopher Critchlow.
"Hukuona kabisa hatari iliyokuwa ikimkabili kwa kuwa peke yake na si kwa sekunde chache tu, bali kwa muda mrefu sana."
Danielle alirudia tena kudanganya, kwanza kwa madaktari akitokwa machozi kuonesha hasira yake, kisha kwa timu ya wahudumu wa dharura, akidai kuwa aliwaacha watoto wake kwa dakika chache tu.
Mama huyo jana ameanza rasmi kutumikia adhabu yake ya kifungo cha miezi 45 jela.

No comments:
Post a Comment