Mahakama Kuu Tanzania, Divisheni ya Kazi imekiamuru Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kusitisha mgomo kutokana na kufanyika kinyume cha sheria.
Aidha, imekitaka chama hicho kulipa hasara kwa mwajiri na fidia kwa wanafunzi iliyosababishwa na mgomo huo, ikiwa ni pamoja na kufidia muda wa masomo wa wanafunzi walioyakosa wakati wa mgomo, hususan kwa wanaotarajia kufanya Mitihani ya Taifa mwaka huu.
Pia wametakiwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuwataarifu walimu kwisha kwa mgomo kama walivyofanya wakati wakiwataarifu kuuanza.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Sophia Wambura baada ya kusoma mwenendo wote wa kesi hiyo inayohusisha mgomo huo uliodumu kwa siku tatu akisema ulikuwa kinyume cha sheria, na hivyo kuamuru walimu wote walioshiriki warudi kazini mara moja.
Alisema kutokana na sheria kukiukwa, na chama hicho kutoa notisi ya saa 48 mwishoni mwa wiki jambo hilo lilifanya mwajiri kushindwa kulinda mali zake kama sheria inavyoagiza.
Jaji Wambura alisema walitoa notisi kwa Serikali, Ijumaa na kuanza mgomo Jumatatu asubuhi huku wakijua kuwa siku za mwishoni mwa wiki hakuna kazi serikalini.
Pia Jaji huyo alisema wakati CWT ikitangaza mgomo, tayari kesi ilikuwa mahakamani, hivyo pamoja na upigaji kura kwa wanachama wake kukubali au kukataa mgomo huo, bado haikuwa sahihi.
Serikali katika kesi hiyo iliwakilishwa na mawakili wawili, ambao ni Wakili wa Serikali Mkuu Robert Msumagu na Pius Mboya huku CWT ikiwakilishwa na Wakili Gabriel Mnyele.
Jaji Wambura alisema pia kulikuwa na kasoro katika taarifa ya mgomo huo, kwani haikuelezwa kisheria ni wa aina gani na kikomo chake, hivyo katika kipengele hicho CWT haikufuata sheria.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Mnyele alieleza kuridhishwa kwake na uamuzi uliotolewa na Mahakama na kuhusu kukata rufaa, alisema hajazungumza na wateja wake.
Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch alisema watazungumza na waandishi wa habari leo saa nne asubuhi kuhusu hukumu hiyo.
Mgomo huo ulianza wiki hii kwa walimu kuacha kuhudhuria shuleni huku wengine wakifika na kusaini kisha kuondoka, ambapo Serikali ilifungua kesi hiyo kutaka mgomo usitishwe kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
Akizungumza na wahariri na wakuu wa vyombo vya habari Ikulu Dar es Salaam juzi, Rais Jakaya Kikwete alisema Serikali inawajali, inawaamini na inatambua mchango wa walimu katika jamii.
Lakini alisema haina uwezo wa kulipa madai ya walimu yanayofikia Sh trilioni 6, yakiwamo ya nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100 na mengine ambayo ni pamoja na asilimia 55 ya mishahara kama posho ya walimu wa masomo ya Sayansi, asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya Sanaa na asilimia 30 ya posho ya mazingira magumu.

No comments:
Post a Comment