Daktari wa zamani wa ngozi wa Michael Jackson, Arnie Klein anakabiliwa na adhabu ya kutojishughulisha na madawa kwa mujibu wa Bodi ya Madawa ambayo imefungua mashitaka kudai kubatilishwa kwa leseni ya Klein.
Mtu anayeshinikiza madai hayo ni Linda Whitney, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo anayeshughulikia Masuala ya Walaji, ambaye anadai Klein amekaidi kufanyiwa upimaji wa lazima wa akili na mwili kwa ujumla, kama sheria za bodi hiyo zinavyoagiza.
Arnie, mmoja wa marafiki wa karibu wa Michael Jackson na nyaraka zinazoonesha kiasi cha kutisha cha dawa alizoshauriwa kutumia mwimbaji huyo, aliamriwa kufanyiwa uchunguzi huo kufuatia malalamiko kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa dhidi ya daktari huyo mwaka 2010, ikidai huduma mbovu isiyokidhi viwango kwa wagonjwa wawili.
Wagonjwa hao hawakutajwa, hivyo haijafahamika kama Michael Jackson ni mmoja wao.
Klein aliamriwa kukabidhi vipimo hivyo vya akili na mwili kwa ujumla hadi kufikia Juni 8, mwaka huu, lakini hapo awali iliripotiwa kwamba daktari huyo aligoma, akitaka kujua ni nani hasa aliyetoa malalamiko hayo.
Sasa, Whitney anaitaka Bodi kuweka shinikizo zaidi katika zoezi hilo la upimaji wake.
Msemaji wa Klein, Joel Douglas ameeleza, "Tuko tayari kutoa ushirikiano, tunachohitaji ni kujua sababu zilizoko nyuma ya uchunguzi huo. Tunaamini mahakama itatenda haki katika hili."

No comments:
Post a Comment