Nyota wa masumbwi Floyd Mayweather ameachiwa huru kutoka Gereza la Las Vegas mapema jana baada ya kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi miwili kwa kumdunda mpenzi wake a zamani mbele ya watoto wao.
Bingwa huyo mtetezi wa mkanda wake kwa mara tano alilakiwa na ndugu zake wapatao 20 na marafiki, akiwamo rapa 50 Cent, wakati alipokuwa akichomoza kutoka gerezani humo mapema alfajiri.
Bondia huyo mwenye miaka 35 alikuwa kimya, kama aliyekuwa gizani, aliingia kwenye gari dogo aina ya Bentley rangi ya bluu ambapo aliendesha mwenyewe kuondoa eneo hilo.
Ametumikia miezi miwili kati ya mitatu jela wakati alipokuwa akimvuta nywele, kumnyonga mikono katika shambulio dhidi ya mpenzi wake wa zamani Josie Harris huku watoto wao wawili kati ya watatu wakishuhudia.
Na sasa yuko huru kuendelea na shughuli zake za ndondi wanasheria wake wameonya kwenye nyaraka mahakamani kwamba yuko kwenye hatari sababu chakula cha jela na maji hayakidhi mahitaji yake ya mpangilio wa mlo.
Pia walisema ukosefu wake wa muda wa kufanya mazoezi kwenye selo yenye ukubwa usiozidi futi za mraba 98 unatishia afya yake na uimara wake.
Mengi yametokea katika ulimwengu wa Mayweather tangu alipohukumiwa kifungo Juni 1, mwaka huu.
Kukiwa hakuna televisheni kwenye chumba chake, hakuweza kumuona mpinzani wake Manny Pacquiao akipoteza mkanda wake wa WBO wa uzito wa kati Juni 9 pale alipopigwa kwa pointi na Timothy Bradley.
Mayweather ambaye amepachikwa jina la utani 'Money', hakuweza pia kuhudhuria sherehe baada ya Jarida la Fobes kumtangaza kuwa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa mwaka 2011.
Na akakosa pia sherehe binafsi ya siku ya kuzaliwa kwa mchumba wake, Shantel Jackson iliyofanyika wiki iliyopita mjini Las Vegas ambapo alialika marafiki zake pekee.
Lakini kwa sasa Mayweather ni mtu huru, hata kama mpinzani wake anayefuata bado hajajulikana wazi kwa sasa.
Meneja wa Mayweather, Leonard Ellerbe hakuweza kupatikana kusema chochote baada ya kugoma kujibu meseji mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari.
Mapromota wa mpinzani mkubwa wa Mayweather, bondia kutoka Ufilipino Manny Pacquiao, wanafanya maandalizi ya pambano kati ya mabondia hao Novemba 10 kwenye Ukumbi wa MGM Grand Garden, mjini Las Vegas, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Michezo Nevada, Keith Kizer.
Mpinzani wa Pacquiao bado hajatajwa lakini Mayweather hafikiriwi kuwamo kwenye orodha hiyo.
Pacquiao ambaye amevuna Dola za Marekani milioni 62 katika mapambano na vyanzo vingine mwaka jana, anashika nafasi ya pili katika orodha Forbes ya wanamichezo tajiri nyuma ya Mayweather ambaye amevuna Dola za Marekani milioni 85 kutokana kwenye mapambano yake.
Ili kuweza kupigana mjini Las Vegas, Mayweather anahitaji kupata leseni mpya kutoka Kamisheni ya Michezo Nevada, alisema Kizer juzi. Leseni yake ya mwisho, kwa ajili ya pambano la Mei 5 dhidi ya Miguel Cotto ilikuwa kwa ajili ya pambano moja tu.
Mayweather amepunguziwa siku 30 kutoka kwenye adhabu yake ya kifungo cha siku 90 jela ili aweze kufanya kazi za kusaidia jamii na kurekebisha tabia yake.

No comments:
Post a Comment