WAMUUA BABA, WAMBAKA MAMA KISHA KUMUUA YEYE NA MWANAE...


KUSHOTO: Amaro Viana akiwa na wazazi wake pamoja na dada yake wa kambo, Gabriela (katikati). JUU: Amaro Viana. CHINI: Genge lililosambaratisha familia ya Viana.
Hata katika nchi inayoshuhudia vifo vya watu 44 kwa siku moja, keshi hii imetisha mno jamii.
Genge la wakabaji limewaua kwa risasi baba, likambaka na kumuua mkewe. Kisha, katika hitimisho unyama wao, wakamzamisha mtoto wa kiume wa wanandoa hao mwenye miaka 12 kwenye maji ya moto.
Amaro Viana aliuawa katika kile kinachoaminika kuepusha kuwatambua waporaji hao ambao walifanya unyama huo katika kitongoji kimoja Afrika Kusini.
Genge hilo linajumuisha mfanyakazi wa bustani wa familia hiyo na mtoto wa mtumishi wa nyumbani.
Ilidaiwa walishawishiwa na jinsi walivyokuwa wakitendewa na familia ya Viana.
Wakiwa mahakamani juzi, mfanyakazi wa bustani Patrick Radebe mwenye miaka 24, akikiri kushirikiana na genge hilo ambalo lilivamia nyumbani hapo Oktoba mwaka jana.
Mahakama ya Mkoa wa Vereeniging ilielezwa kwamba, baada ya kuweza kuingia ndani ya nyumba hiyo iliyoko huko Walkerville, kitongoji kilichoko mjini Johannesburg, genge lilimsubiri baba wa Amaro, Tony ambaye ni mhandisi mwenye miaka 53, awasili nyumbani.
Alipoingia kupitia mlango wa mbele, walimshambulia kwa fimbo za kuchezea gofu na visu vinavyofanana na mapanga kabla ya kumfunga na kumwamuru awaeleze jinsi ya kufungua kasha la kuhifadhia pesa.
Wakati mke wa Viana, Geraldine mwenye miaka 43, na mtoto wake kurejea nyumbani hapo, nao wakavamiwa na kushambuliwa pia.
Mama na mtoto walifungiwa kwenye vyumba viwili tofauti.
Kisha wanaume wawili kati ya hao wakambaka mke wa Viana kabla ya wote, yeye na mumewe kupigwa risasi na kufa.
Kwa mujibu wa kukiri kwao mahakamani, Radebe na mwenzake Sipho Mbele mwenye miaka 21, walijua kwamba endapo mtoto wa wanandoa hao akiachwa hai, angeweza kabisa kuwatambua na kuwataarifu polisi.
"Tulienda bafuni na kufungulia bomba," taarifa ya wawili hao ilisomeka, "Tulimziba mdomo sababu alikuwa akilia. Tulimzamisha kwenye bafu uso chini, tukiamini angezama na kufa."
Mbwa wa familia ya Viana pia aliuawa pale tumbo lake lilipochanwa kwa kisu.
Kwa bahati binti wa Viana aliyempata kutoka katika ndoa yake ya kwanza, Gabriela, hakuwapo nyumbani hapo kwa baba yake wakati waporaji walipovamia.
Licha ya kuimarika kwa udhibiti wa idadi ya matukio ya uhalifu, Afrika Kusini imebaki kuwa moja ya nchi hatari zaidi duniani.
Wastani wa chini ya watu 44 kwa siku wanauawa hapa.
Hii ni kulinganisha na 1.5 nchini Uingereza na Wales, ambazo zina idadi ya watu inayolingana.
Mbali na ukanda wa vita, kiwango cha mauaji Afrika Kusini kinazidiwa na mataifa ya Amerika Kusini pekee ambavyo vinahamasishwa na mapigano kati ya magenge yanayojihusisha na dawa za kulevya.
Dianne Kohler Barnard, waziri kivuli wa Polisi, alisema mauaji ya familia ya Viana yalikuwa 'ya kutisha'.
"Wanawake wanabakwa na watu wanauawa kwa risasi kila siku," mwanasiasa wa Upinzani wa Democratic Alliance alisema. "Lakini ukweli ni kwamba mauaji ya mtoto wa miaka 12 yanatisha. Yalishitusha."
Mbele na Radebe walipatikana na hatia katika mashitaka ya uvunjaji kwa lengo la kuiba, uporaji, ubakaji, mauaji ya watu watatu, kumiliki silaha, kumiliki vifaa vya maangamizi kinyume cha sheria na dhamira ya kuharibu mali.
Wakili wa waathirika hao, Charmaine Castleman alidai wanaume hao walifanya shambulio kama namna ya kulipiza kisasi kwa jinsi mke wa Viana alivyokuwa akiwatendea siku zilizopita.
Akielezea tukio la ubakaji alisema: "Kwanza Mbele alimbaka huku Radebe akimsaidia kumshikia wakati akiwa kasimama kichwani.
"Kisha Radebe akambaka huku Mbele akiwa kamziba usoni kwa kutumia mto."
Mfuasi wa tatu wa genge hilo, Sphiwe David Motaung mwenye miaka 20, hapo kabla alipatikana na hatia ya uporaji wenye lengo la kuiba, uporaji wa kutumia nguvu na kuharibu mali.
Kwa mujibu wa ripoti mojawapo walirejeshwa rumande huku wakiwa wanatabasamu baada ya kutoka mahakamani.

No comments: