WANYONG'ONYEZWA NA TAARIFA ZA KIFO CHA GRIFFITH...

Watu wanaoendesha Makumbusho ya Andy Griffith mjini Mount Airy huko North Carolina wameelezea 'kukatishwa tamaa' kwao na taarifa za kifo cha gwiji huyo wa televisheni wakisema "Tumebarikiwa mno kumfahamu."
Tanya Jones ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Surry ambaye pia anasimamia Makumbusho ya Andy Griffith, yanayojumuisha mkusanyiko mkubwa wa kazi za Andy Griffith duniani.
Tanya amesema, "Andy Griffith ni kila kitu katika ulimwengu wa sanaa kokote uendako, si hapa tu Mount Airy. Mchango wake kwetu, Baraza la Sanaa la Surry na mji wa Mount Airy haupimiki."
Sliongeza, "Tumebarikiwa sana kumfahamu. Tutaziheshimu kazi zake za sanaa, muziki wake, kipaji chake na pia Kipindi chetu tukipendacho cha Andy Griffith Show."
"Sala zetu na upendo wetu tunaukabidhi kwa Cindi. Tunaamini kwamba Andy yuko mahali pema na hicho ndicho kitu muhimu kwa sasa."

No comments: